Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 April 2014

MVUA KULETA MAAFA ZAIDI DAR

Foleni jijini Dar inayosababishwa na kuharibika kwa miundombinu kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, zimeendelea kuleta maafa, ikiwamo vifo na uharibifu wa miundombinu, huku safari hii yakihusisha mawasiliano ya barabara kati ya vijiji vya Ibungu na Ndandalo kwenda mjini Kyela kukatika, baada ya daraja la Mto Kiwira linaloyaunganisha kuzolewa na mafuriko.

Daraja hilo liling’olewa juzi na kusababisha wakazi wa vijiji hivyo kushindwa kuvuka mto huo kwenda kupata mahitaji yao mjini Kyela.

Mbali na kuvunjika kwa daraja hilo, mvua hizo pia zimeleta maafa makubwa  katika maeneo mbalimbaliya wilayani hapa ikiwa ni pamoja na baadhi ya nyumba kubomoka na mazao kusombwa na maji.

Diwani wa Kata ya Ikimba, Haleluya Mwakaseja, alisema hali ni mbaya kwa wakazi wa vijiji hivyo, kwani wameshindwa kuvuka mto huo na kwamba, haijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Alisema amewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga, na wahandisi wa halmashauri ili kurejesha mawasiliano ya barabara katika vijiji hivyo.

WENGINE WAFA MAJI 
Katika hatua nyingine, msichana aliyetambuliwa kwa jina moja la Jamila amekutwa amekufa baada ya kutumbukia na kuzama katika mto Mwakyela wakati akijaribu kuvuka, juzi saa 1:00 asubuhi, tukio lililothibitishwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bondeni, mjini Kyela, Wille Fumbo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Kitonga, Omary Abbas (14), ambaye maiti yake ilikutwa ikielea katika mto Mzinga, eneo la Kilakala Yombo, juzi saa 12:30 jioni.

Kiondo alisema marehemu alikutwa na umauti wakati akijaribu kuvuka mto huo kwa kuogelea, lakini maji yalimzidi nguvu.

Pia alisema mwili wa Omary Jumbe Benjamini (15) ulikutwa ukielea ndani ya maji katika mashimo ya mchanga, yaliyopo Mbande, juzi saa 11:00 jioni.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili na alitoweka nyumbani kwao bila kuaga hadi pale mwili wake ulipookotwa.

TMA: MSIRUDI MAENEO HATARISHI
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi, amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko kutokurudi katika maeneo hayo kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha.

Alisema mvua zinazoendelea kunyesha ni za msimu wa masika, ambazo katika Ukanda wa Pwani ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na visiwa vya Unguja, zitaendela kunyesha hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao.

Dk. Kijazi alisema kiwango cha mvua hizo, historia inaonyesha kuwa ziliwahi kutokea mnamo mwaka 1968 zikiwa za ujazo wa milimita 136.9, huku za mwaka huu zikifikia milimita 138.1 kutoka katika kipimo kilichochukuliwa katika Uwanja wa Ndege wa KImataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Aprili 11.

WASHINDWA KWENDA SHULE
Wakati TMA ikitoa tahadhari hiyo, wakazi wanaoishi mabondeni waliokuwa wamejihifadhi katika jengo la Klabu ya Yanga, wamerejea katika makazi yao ya zamani, huku wakilalamika kukosa chakula na malazi na watoto wao wakishindwa kwenda shule kwa madai kwamba, nguo zao zimezolewa na maji.

Wakizungumza na NIPASHE jana walisema hadi sasa hakuna taasisi yoyote iliyojitokeza kuwasaidia na kuishi maisha magumu kutokana na mali zao kusombwa na maji na wengine kuibiwa na vibaka wakati maji yalipoingia.

FOLENI DAR BALAA
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha foleni kubwa maeneo ya katika ya jiji.

Imeandikwa na Enles Mbegalo, Hussein Ndubikile, Christina Mwakangale, Damian Ndelwa, Pilly Nashon, Theonest Bingora (Dar), Grace Mwakalinga (Kyela).
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment