Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 April 2014

HANS POPE AOKOA JAHAZI SIMBA SC

Zacharia Hans Pope

Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya Simba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspoppe jana amesaidia fedha za mishahara ya wachezaji ambao waligoma kwendaZanzibar bila ya kulipwa.

Mjumbe huyo ametoa zaidi ya Sh. milioni 30 kusaidia malipo hayo kutokana na wachezaji kukataa kwenda Zanzibar bila kulipwa mishahara yao na posho kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya kukamilisha ratiba dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Habari ambazo gazeti hili imezipata zimeeleza kuwa baada ya leo asubuhi wachezaji kumaliza mazoezi walitakiwa kuelekea bandarini lakini nyota hao waligoma mpaka madai yao yalipofanyiwa kazi.

Kufuatia hali hiyo, kikosi cha nyota 18 walioteuliwa kwenda Zanzibar kililazimika kuahirisha safari asubuhi na badala yake kimeondoka boti ya saa tisa mchana.

"Hanspoppe ndiyo ameokoa jahazi wachezaji waligoma hadi walipolipwa...aibu sana," kilisema chanzo chetu.

Fedha hizo zilizotolewa wamelipwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi mshahara wa mwezi uliopita.

Awali benchi la ufundi lilipendekeza timu iingie kambini juzi Jumanne lakini ilishindikana kutokana na kukosa fedha.

Hanspoppe amekataa kuzungumzia hali hiyo iliyotokea ndani ya klabu.

Wachezaji walioondoka kuelekea kambini Zanzibar ni pamoja na Ivo Mapunda, Yaw Berko, WilliamLucian, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba, Amissi Tambwe, Said Ndembla na Ramadhan Singano.

Nyota wengine ni Nassor Masoud 'Chollo', Henry Joseph, Ramadhan Chombo ' Redondo', Uhuru Selemani, Awadh Juma na Zahor Pazi.

Simba na Yanga zinawania kushinda mechi hiyo ili kulinda heshima baada ya bingwa wa msimu huu, Azam FC, kuwa ameshapatikana.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment