Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 4 June 2014

TANZANIA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO KASI – PINDA

PG4A1221Waziri Mkuu, izengo Pinda  akifungua Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit) kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam,  Juni 3, 2014. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A1269Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijiniDar es salaam Juni 3, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A1241Waziri Mkuu,, Mizengo Pinda akizungumza na   Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Philippe Dongier baada ya kufungua Mkutano waMajadiliano wa kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo  haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam  Juni 3, 3014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda  amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia nasekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho (Jumatano, Juni 4, 2014).
 Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji inakua kwa kasi barani Afrika.
 ”Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo,” alisema.
 Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Jiji la Dar es Salaam.
“Hii ni awamu ya kwanza ambayo inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi kuelekea maeneo tofauti ya Jiji,” alisema.
Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
“Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni kuimarisha tu usafiri huu,” aliongeza Waziri Mkuu.
Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa.
Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
 kutano huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za maduka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMANNE, JUNI 3, 2014.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment