Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 10 April 2014

UKITAKA NYAMA YA MBUZI, UTAIPATA HAPA

 Naam. Kama unasafiri kwa barabara ya kati, yaani Dar-Dodoma-Mwanza, hakika kwa wale wanaohitaji nyama ya mbuzi iliyochomwa vizuri, basi wataipata pale Mbande, njiapanda ya kwenda Kongwa. Hata kama hukuipata ya kuchoma, bado unaweza kuondoka na paja ambalo utalibanika huko uendako.
 Mitaji ni changamoto, lakini vijana wanaweza kubuni shughuli mbalimbali za kujiajiri, kama huyu anayechoma nyama hapa Mbande. Nimenunua kiasi na kutafuna nikiwa safarini.
 Vichwa hivi vya mbuzi ni kielelezo kwamba nyama inayochomwa hapo siyo ya porini wala siyo kibudu. Imepimwa na kuthibitishwa na bwana mifugo. Hata hivyo, bado navyo ni biashara. Zamani vichwa na makanyagio vilikuwa vinagawiwa kwa mchinjaji, lakini sasa kila kitu pesa.
 Biashara inaendelea kama kawaida, kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa saba usiku.
 Naam, kijana akiniandalia nyama kidogo ya kutafuna.
Kazi mtindo mmoja.

No comments:

Post a Comment