Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 16 April 2014

MAKAMBA: KWA SERIKALI TATU, TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZITAGAWANA MADENI

January Makamba

Dodoma. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Yusuf Makamba amesema mfumo wa serikali tatu ukikubalika na kupitishwa kuongoza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  wajumbe wafahamu kuwa ndani ya miaka miwili Muungano utakuwa umevunjika.
Makamba alikuwa akichangia mjadala bungeni juzi jioni, kuhusu sura ya kwanza na sita ya Rasimu ya Katiba ambazo tayari zimefanyiwa kazi na Bunge hilo, kupitia kamati zake 12.
“Kama tunataka Muungano wetu uvunjike ndani ya mwaka mmoja hadi miwili, basi ndugu mwenyekiti tuingie katika muundo wa serikali tatu,” alisema.
Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli, alisema kuwa Muungano utakuwa janga kwa kuwa anaufananisha na lulu. Alisema nchi nyingi za Afrika zimetengenezwa kwa mipaka ya wakoloni, tofauti na Tanzania ambayo imejitengenezea kitu chao na wao wenyewe wakakipa jina kwa kukiita Tanzania,” alisema Makamba.
Makamba alisema ikiwa sasa Watanzania wanataka dunia iwacheke, waue Tanzania waliyoitengeneza. Alisema baada ya Katiba kupitishwa, mambo yatakayofanywa na nchi itapokuwa katika kipindi cha mpito ni pamoja na kugawana mali, madeni na watumishi, kitendo alichosema kuwa ni cha utengano.
“Kwenye kitendo cha kugawana mali, watu na madeni hapo hapo ndipo itakapokuwa mwisho wa Muungano. Ina maana mapendekezo ya rasimu hii yakipitishwa, Tanzania ndani ya miaka miwili itakuwa ikishughulikia mgawanyo wa mali,” alionya.
Makamba alisema wengi wa vijana kama yeye wanatarajia kuongoza Tanzania na kwamba hawako tayari kupokea nchi ikigawana mali, madeni na watu kwa kuwa wana ndoto nyingi za kufanya Tanzania kuwa moja ya mataifa kubwa barani Afrika.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment