Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 16 April 2014

LOGA AKAMIA USHINDI YANGA

Kocha Mkuu wa Simba, Logarusic

Kocha wa timu ya Simba, Mcroatia Zdravco Logarusic amesema kuwa anahitaji kupata ushindi katika mechi ya funga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wa jadi Yanga ili kuokoa kibarua chake ndani ya timu hiyo.

Simba imekuwa na msimu mbaya baada ya kupoteza mechi sita na kutoka sare 10 katika mechi zao 25 walizocheza katika ligi msimu huu, na ilianza mzunguko wa pili kwa kumfukuza aliyekuwa kocha wao Abdallah 'King' Kibadeni na kumleta Mcroatia huyo ambaye ameshindwa kubadili mwenendo mbovu wa timu hiyo.


Hadi sasa Simba iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 37, ikizidiwa na mabingwa Azam kwa pointi 22 na imepitwa na mahasimu wao Yanga walio katika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 18.

Logarusic aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa anataka timu yake ishinde ili kuendeleza heshima na kulinda ajira yake.

Kocha huyo alisema kuwa anajua mchezo huo utakuwa ni mgumu baina ya miamba hao wa soka nchini ambao msimu huu wametoka kapa baada ya timu zote mbili kuukosa ubingwa wa bara uliotua kwa Azam FC ikiwa imebaki mechi moja ligi kumalizika.

Aliongeza kwamba pia ushindi utawaongezea umoja na kujipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao.

"Tunahitaji kushinda na wao Yanga wanahitaji ushindi...ila wao watashuka wakiwa na machungu ya kuvuliwa ubingwa na Azam," alisema kocha huyo.

Aliwataka wachezaji watakaopata nafasi siku ya Jumamosi kuonyesha kiwango cha juu ili watimize malengo ya kupata ushindi.

Alisema kuwa anasikitika timu yake kuukosa ubingwa msimu huu licha ya kuanza vyema mzunguko wa kwanza ilipokuwa chini ya kocha mkuu, Abdallah Kibadeni.

Simba kwa mwaka wa pili mfululizo imekosa tiketi ya kushiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Kikosi cha Simba sasa kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea Zanzibar kujiandaa na mchezo huo dhini ya mtani wake ikiwa na nyota 18.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Selemani Matola, alisema jana kwamba wamefanya mabadiliko ya safarikutokana na maelekezo waliyopewa na uongozi wa klabu hiyo.

Matola alisema timu ilifanya mazoezi asubuhi na baada ya kumaliza programu nyingine jana jioni ndiyo walitarajia kuteua wachezaji watakaokwenda Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment