John Heche
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wabunge
wa Bunge Maalumu la Katiba (BMK) wanaounda Umoja wa kutetea Katiba ya
Wananchi (UKAWA) walisusia vikao vya bunge hilo kwa sababu ya CCM kwa
upande mmoja na serikali yake kwa upande mwingine kuendeleza vitendo vya
kupanda chuki, ubaguzi wa waziwazi wa kikabila na dini, matusi pamoja
na kuacha rasimu ya wananchi na kupenyeza rasimu ya CCM ndani ya bunge
maalumu la Katiba.
Baraza
la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) linapongeza kwa dhati hatua hii ya
kuachana na Bunge ambalo kimsingi linaonekana kuwa hatari kwa umoja,
mshikamano na amani ya Taifa letu.
Lugha
za ubaguzi wa waziwazi wa kidini zilizotelewa na viongozi wa serikali
na CCM ni sumu mbaya kwa taifa hili kwani kundi linalobaguliwa likikosa
uvumilivu tutalishuhudia taifa letu likitumbikia kwenye machafuko kama
yale yanayoendelea kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutibu donda kama
hilo daima haiwezekani kama historia inavyotuasa.
Aidha
kubagua watanzania kwa makabila yao ni kitendo haramu kichopaswa
kukomeshwa mara moja kwani hii ni chemikali mbaya isiyo na kifani kwa
umoja wa Taifa letu.
Hivyo
ni mwendawazimu pekee angekubali kushiriki dhambi hii mbaya na
isiyosameheka ya kulipasua taifa na kuhujumu maoni ya wananchi wanaotaka
mabadiliko ya taifa lao kupitia Katiba mpya iliyokua ikiendelea ndani
ya BMK.
BAVICHA
inaamini kuwepo kwa hali ya namna hii inayojitokeza kwenye mchakato wa
Katiba mpya kunatokana na udhaifu wa Rais Kikwete kama kiongozi wa nchi
ambaye , kwa kuruhusu mawaziri wake na wbunge wa chama chake kufanya
vitendo hivi, amekubali taifa limfie mikononi mwake.
Rais
Kikwete kuasisi na kuzikubali lugha za vitisho dhidi ya wananchi
wanaotaka mabadiliko kwenye muundo wa serikali ya Muungano kupitia yeye
mwenyewe, mwaziri na viongozi mbalimbali wa serkali na chama chake
kunadhihirisha jinsi asivyojali na alivyodhamiria kulipasua vipande
vipande taifa hili.
Wakati
BAVICHA tukiunga mkono na kupongeza juhudi za UKAWA za kuzunguka nchi
nzima kuwaelimisha wananchi juu ya uchakachuzi na hujuma dhidi ya maoni
yao zinavyofanywa na serikali na CCM, pia tunataka mambo ya fuatayo
yafanyike;
1.
Jakaya Mrisho Kikwete kama Rais aombe radhi taifa kwa lugha zake za
vitisho alizozitoa wakati akizindua BMK kwani kauli yake haikua na
tafsiri nyingine zaidi ya kuwa rasimu ya wananchi ikipita kama ilivyo
basi ataliamuru Jeshi kuchukua mamlaka. Kauli kama hii haikupaswa kutoka
kwenye kinywa cha mtu mwenye hadhi kama ya rais.
2.
Jakaya Mrisho Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM atoke sasa hadharani
aliombe taifa msamaha kwa vitendo vichafu na viovu vinavyofanywa na wana
CCM na mawaziri wake ndani na nje ya BMK. Sambamba na hilo, ili
kurudisha imani na mshikamano ndani ya taifa letu, Kikwete akemee
hadharani wabunge wa CCM na washirika wake kukoma mara moja tabia hii
ambayo sio tu ni mbaya bali pia ni ya hatari kwa taifa letu.
3.
Waziri Mkuu aliyemtuma waziri LUKUVI kwenda kuhubiri udini kwenye
madhabau ya nyumba za Ibada na ndani ya BMK kwa niaba yake aombe radhi
taifa kwa kitendeo hicho kwani kwa vyovyote vile haitarajiwi kiongozi wa
serikali kupanda chuki za namna hii miongoni wa wananchi wa taifa letu.
4.
Kwa kua mpaka sasa waziri Lukuvi, kwa kauli zake ameonekana kuwa kirusi
cha hatari kwa umoja, mshikamano na amani ya taifa letu, ni vema na
muhimu akafukuzwa kwenye nyadhifa zake zote.
5.
Kwa kua tume aliyoiteua Rais Kikwete ya kukusanya maoni ya wananchi juu
ya Katiba mpya iliundwa na watu waliokuwa na wanaoheshimika kwa
utumishi wao ndani na nje ya taifa na ambao kwa uadilifu wao wamefanya
kazi yao kama ilivyostahili hata kama haiipendezi serikali na CCM,
waombwe radhi na Rais Kikwete mwenyewe hadhari kwa matusi waliotukanwa
na wabunge na viongozi mbalimbali wa CCM ndani nan je ya BMK. BAVICHA
inaamini hata mtu angekua amepungukiwa na akili kiasi gani, matusi
yaliyoelekezwa kwa wazee kama wakina Warioba, Butiku, Ahmed Salimu, Jaji
Ramadhani, Prof Baregu na wengine hayavumiliki kwa kiwango chochote
kile
Imetolewa leo tarehe 20.04.2014 Jijini Dar es salaam na;
John Heche
Mwenyekiti Taifa - BAVICHA
Mwenyekiti Taifa - BAVICHA
No comments:
Post a Comment