Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
ZAIDI ya wanawake 100 wa Kanisa la Sinai Healing Center lililopo ngusero wamenufaika bure na elimu ya ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbali mbali zitakazowawezesha kuachana na hali ya utegemezi kwa waume zao.
Aidha wanawake wakiacha kuwa tegemezi taifa la kesho litaendelea tofauti na sasa ambapo wengi wao wamekuwa magolikipa hali inayoangusha familia zao na taifa kwa ujumla.
Nabii Debora Haruna wa kanisa hilo alisema kuwa yeye aliamua kuchukua jukumu hilo la kujifunza kutengeneza bidahaa mbali mbali na hatimaye akajitolea kuwafundisha wanawake hao ili kuwawezesha kujikwamua katika hali ngumu ya maisha.
Alieleza kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo ya kutoa elimu hiyo ya ujasiriamali alikuwa anapokea malalamiko toka kwa wanawake hao kuwa hawajaachiwa matumizi na waume zao huku wengine wakishindwa hata kuhudumia familia zao kutokana na wao kukosa shughuli za kuwaingizia kipato.
Nabii Haruna aliongeza kuwa kutokana na elimu hiyo aliyowapatia akinamama hao imeasaidia klwa kiwango kikubwa kuwasaidia kuweza kujikimu kimaisha huku wakiweza hata kuwasaidia wanaume zao katika kuendeleza familia zao tofauti na hapo awali walipokuwa wakisubiria tu kutoka kwa wanaume.
“Hawa wanawake nimewafundisha ujasiriamli ili wasaidiane katika maisha kwa kuwa waliumbwa kama wasaidizi na sio magolikipa hali itasaidia sana hata familia zao kuinuka haraka kutokana na vipato wanavyojipatia kutokana na hizi bidhaa wanazozitengeneza wenyewe,” aliongeza Debora.
Alizitaja bidhaa wanawake hao walizonufaika kuzitengeneza kuwa ni pamoja kutengeneza batiki, sabuni za maji, keki za harusi, gesi, mishumaa,shampoo,
Vile vile nabii alieweza kutoa elimu hiyo ya ujasiriamali pamoja na mitaji kwa watoto wenye umri wa kuanzia mika 15 hadi 17 ili kuwawwezesha kuepuka vishawishi wanavyokumbana navyo kwa kuwa mara nyingi watoto haswa wa kike wanadanganyikana kutokana na wao kukosa huduma wanazostahili hivyo kupitia mitaji hiyo itawawezesha kujikimu kimaisha.
No comments:
Post a Comment