Tarehe kama ya leo mwaka 1965 mgodi wa makaa ya mawe wa Yamano jirani na Fukuoka, Japan ulilipuka na kuua watu 236. Janga hilo lingeweza kuepukwa kama waendeshaji wa mgodi huo wangeweka hata tahadhari za msingi. Miaka sita nyuma, wachimbaji saba walipoteza maisha yao na wengine 24 kujeruhiwa vibaya kwenye mgodi huo kutokana na kutokuwepo na njia za kiusalama. Lakini bado Juni Mosi, 1965, jumla ya wachimbaji 559 waliingia kwenye mgodi ambao haukuwa na vipimo vya methanometer – ambavyo vinatumika kudhibiti kiwango cha mentane – wala kuwa na ving’amuzi vya colorimetric, ambavyo vinabaini kiwango cha kemikali kwenye hewa. Yoshio Sakarauchi, waziri wa biashara na viwanda wa Japan, alijiuzuru kwa kashfa hiyo.
JUNI 1, 1980 – CNN YAANZA RASMI
KATIKA tarehe kama ya leo mwaka 1980, Kituo
cha Luninga cha CNN (Cable News Network) cha Marekani, ambacho ni cha kwanza
kabisa duniani kurusha matangazo yake kwa saa 4, kilianzishwa rasmi. Kituo
hicho kilianza kurusha matangazo hayo majira ya saa 12 za jioni kwa saa za
Mashariki – EST (saa 8 usiku kwa saa za Afrika Mashariki) yakitokea kwenye
makao yake makuu jijini Atlanta, Georgia. Habari iliyoongoza siku hiyo ni
jaribio la kutaka kuuawa kwa kiongozi na mtetezi wa haki za binadamu Vernon
Jordan. CNN ilibadili mtazamo kwamba taarifa zinaweza kutangazwa kwa wakati
maalum tu kwa siku. Wakati CNN inaanzishwa, habari za luninga zilikuwa
zimetawaliwa na vituo vikubwa vitatu - ABC, CBS and NBC- ambazo zilikuwa
zinatangaza kwa dakika 30 tu usiku. Awali ikitazamwa na Wamarekani milioni
mbili tu majumbani, kwa sasa CNN inatazamwa na Wamarekani milioni 89 na zaidi
ya watazamaji milioni 160 ulimwenguni kote.
CNN ilikuwa wazo la Robert "Ted"
Turner, mfanyabiashara aliyeitwa “Mdomo wa Kusini”. Turner alizaliwa Novemba
19, 1938 mjini Cincinnati,Ohio, na familia yake ilihamia Georgia akiwa motto mdogo ambapo baba
yake alikuwa anamiliki kampuni kubwa ya matangazo ya mabango. Baada ya baba
yake kujiua mwaka 1963, Turner alichukua jukumu la kuiongoza kampuni hiyo.
Mwaka 1970 alinunua kituo cha televisheni cha Atlanta ambacho kilikuwa
kinaelekea kufa, kikiwa kinatangaza filamu za zamani, lakini yeye akakiimarisha
na kuwa kikubwa. Turner pia alinunua timu ya baseball ya Atlanta Braves na ile
ya mpira wa kikapu ya Atlanta Hawks na kuonyesha michezo yake kwenye kituo cha
TBS (Turner Broadcasting System).
HABARI ZA MAUAJI KWENYE KAMBI YA JESHI WAKATI WA VITA KUU YA PILI
ZAJULIKANA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA
Mojawapo ya magari yaliyotumiwa na utwala wa Kinazi wa Hitler kuwaua Wayahudi huko Chelmno, Poland.
Tarehe kama ya leo mwaka 1942, gazeti
change la mjini Warsaw, Poland, Liberty Brigade, linaripoti hadharani
taarifa za kuuawa kwa gesi ya sumu kwa makumi ya maelfu ya Wayahudi huko Chelmno,
kambi ya mauaji nchini Poland—karibu miezi saba baada ya zoezi la kuwaua
wafungwa kuanza wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Mwaka mmoja nyuma, ulikuwa
umeanzishwa mpango wa "Final Solution," wa kuwaua Wayahudi wa Ulaya
ambapo Wayahudi 700 waliuawa kwa gesi ya sumu kwenye gari ambamo walikuwa
wakisafirishiwa kupelekwa katika kijiji cha Chelmno, Poland. Gari hili la gesi
ndilo likaja kuwa chemba ya mauaji ya Wayahudi 360,000 kutoka katika jumuiya
200 nchini Poland. ‘Faida’ ya mauaji hayo ilikuwa ni ya kimya kimya na
haikuonekana.
Mwezi mmoja kabla ya mkutano wa Wannsee
wa mwezi Januari 1942, ambapo maofisa wa Kinazi waliamua kuzungumzia rasmi
mauaji ya Wayahudi, magari ya gesi ya sumu huko Chelmno yalitumika kuua hadi
Wayahudi 1,000 kwa kutwa.
Mnamo Juni 1, 1942, habari ya kijana
wa Kiyahudi, Emanuel Ringelblum, (ambaye alitoroka kwenye kambi ya mauaji huko Chelmno
alikokuwa amelazimishwa kuzika miili ya watu waliokuwa wanamwagwa na magari
yenye sumu), ikachapishwa na gazeti change la Kisoshalisti nchini Poland la Liberty
Brigade. Ndipo Mataifa ya Magharibi yalipobaini unyama uliokuwa ukifanywa
na Wanazi.
BENEDICT ARNOLD AFIKISHWA MAHAKAMANI WAKATI WA MAPINDUZI YA MAREKANI
Usikilizaji wa kesi ya Benedict Arnold ulianza huko Philadelphia, Pennsylvania.
Baada ya kuonekana na rekodi safi huko nyuma mwanzoni mwa Mapinduzi ya Marekani,
Arnold akashtakiwa kwa makosa 13 ya ukosefu wa uadilifu, ikiwemo kutumia vibaya
magari ya serikali na kununua na kuuza vitu kwa magendo.
Japokuwa Arnold alifutiwa mashtaka yote,
Jenerali George Washington akatoa amri ya kumweka ndani.
Wakati akiwa safarini katika kituo muhimu cha West
Point kuona namna wanavyoweza kukabiliana na majeshi ya Uingereza, Arnold
aliamua kumpuuza Washington na Wamarekani. Aliona kwamba hakuwa amezawadiwa au
kushukuriwa kutokana na mafanikio yake ya kijeshi kwenye vita hivyo. Akaanza
kuwasiliana na majasusi wa Uingereza kwa lengo la kuasi ili West Point iingie
mikononi mwa Waingereza ambao tayari walikuwa wanaushikilia mji wa New York,
hivyo kwa kuutwaa West Point wangeweza kuwa na nafasi ya kuzuia majeshi ya
Marekani yaliyokuwa New England.
Mnamo Agosti 1780, Sir Henry Clinton alimpatia
Arnold Pauni 20,000 kwa kuwapatia Waingereza askari 3,000 wa Marekani pamoja na
kuusalimisha West Point. Arnold akamweleza Jenerali Washington kwamba West
Point ilikuwa tayari kukabiliana na Waingereza wakati ukweli haukuwa hivyo. Pia
alijaribu kuweka mtego wa kukamatwa kwa Jenerali Washington, mpango huo
ungeweza kufanikiwa lakini taarifa yake ilichelewa kuwafikia Waingereza na
Washington akatoroka. Mpango wa West Point kuangukia mikononi mwa Waingereza
nao ulifeli wakati kanali mmoja wa Marekani alipopuuza amri ya Arnold ya kutoishambulia
meli ya Waingereza.
Siri ya Arnold kusailiti ilifahamika kwa
Wamarekani wakati ofisa mmoja wa Uingereza John André, aliyejifanya kama
mesenja, alipokamatwa na kikosi cha AWOL cha Wamarekani waliokuwa msituni
kaskazini mwa New York City.
WAJERUMANI
WASHAMBULIA VIKOSI VYA UINGEREZA YPRES SALIENT
SIKU kama ya leo mwaka 1916, wakati
vikosi vya wanamaji vya Ujerumani na Uingereza vilipopambana katika Bahari ya
Kaskazini wakati wa Vita ya Jutland na Wafaransa wakipambana kuhakikisha
Wajerumani hawautwai mji wa Verdun, vikosi vya Ujerumani vikaanzisha
mashambulizi makubwa dhidi ya Uingereza huko Ypres Salient katika eneo la Western
Front. Hii ilikuwa na wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
KAMPUNI YA MAGARI YA NISSAN YAANZISHWA
Juni Mosi kama leo, mwaka 1934, kampuni ya Jidosha-Seizo
Kabushiki-Kaisha (kwa Kiingereza Automobile Manufacturing Co., Ltd.) ya jijini Tokyo, yapata jina jipya
na kuitwa: Nissan Motor Company.
Jidosha-Seizo Kabushiki-Kaisha ilianzishwa
Desemba 1933. Nissan ilitengeneza gari lake la kwanza aina ya Datsun kwenye
mtambo wake wa Yokohama mnamo Aprili 1935 na mwaka huo ikaanza kusambaza magari
yake kwenda Australia. Kuanzia mwaka 1938 hadi wakati wa Vita Kuu ya Pili ya
Dunia, Nissan ikaanza kutengeneza malori na magari ya vita. Majeshi ya
Washirika yalikiteka kiwanda cha Nissan mwaka 1945 na hayakukirejesha hadi
miaka kumi baadaye.
Mwaka 1960, Nissan ikawa kampuni ya kwanza ya
magari ya Kijapani kutwaa tuzo ya Uhandisi ya Deming. Aina mpya ya magari ya
Datsun kama Bluebird (1959), Cedric
(1960) na Sunny (1966) yaliweza kuongeza mauzo ya Nissan ulimwenguni.
WAMUUNGA MKONO NIXON VIETNAM
Jun 1, 1971: Tarehe kama ya leo
mwaka 1971 kundi la Vietnam Veterans for a Just Peace linajitokeza hadharani
kuunga mkono uamuzi wa Rais Richard Nixon wa kuendesha vita vya Vietnam.
VIGOGO WAKUTANA KUJADILI VIETNAM
Tarehe kama ya leo mwaka 1964 maofisa wa juu wa Marekani wakutana mjini
Honolulu kwa siku mbili kujadiliana kuhusu Vita ya Vietnam. Waliohudhuria ni
pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Dean Rusk, Waziri wa Ulinzi Robert McNamara,
Balozi Henry Cabot Lodge, Jenerali William Westmoreland, Jenerali Maxwell
Taylor, na Mkurugenzi wa Idara ya Kijasusi ya Marekani (CIA) John McCone.
Mjadala huo ulihusisha hali ya vita Kaskazini mwa Vietnam, ikiwemo maeneo 94
muhimu ya kushambulia.
VITA YA COLD HARBOR YAANZA
Tarehe kama ya leo mwaka 1864, majeshi ya
Uingereza (Confederates) anavishambulia vikosi vya Union katika eneo la Cold
Harbor, Virginia, karibu maili 12 kutoka Richmond. Hii ilikuwa wakati wa Vita
vya Mapinduzi.
Tangu kuanza kwa mwezi Mei 1864, Jenerali wa
Jeshi la Union Ulysses S. Grant alikuwa amejipanga
kulishambulia Jeshi la
Robert E. Lee Kaskazini mwa Virginia karibu na Richmond. Hali hiyo ilikuwa na
madhara kwa Jeshi la Grant huko Potomac, ambapo watu 60,000 waliuawa.
URUSI YAMSHTAKI SHCHARANSKY KWA UHAINI
Tarehe kama ya leo mwaka 1977 wakati wa Vita
Baridi, serikali ya Urusi ilimfungulia mashtaka ya uhaini Anatoly Shcharansky, kiongozi
wa kutetea hali za Wayahudi na mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Russia.
Kitendo hicho kilitazamwa na mataifa ya Magharibi kama changamoto ya moja kwa
moja kwa Rais wa Marekani Jimmy Carter kuhusiana na sera yake mpya ya mambo ya
nje kuhusu haki za binadamu na kupinga ukandamizaji wa Urusi.
Shcharansky, aliyekuwa na miaka 29 na mtaalam
wa kompyuta, alikuwa mashuhuri katika kundi lililojiita ‘Helsinki Group’ katika
Muungano wa Kisovieti. Kundi hilo lilianzishwa mwaka 1975, baada ya kusainiwa
kwa Sheria ya Usalama ya Ulaya (European Security Act) ambayo pia inajulikana
kama Helsinki Accords. Mkutano huo uliofanyika jijini Helsinki, Finland
uliwahusisha viongozi wa Marekani na Urusi ambao waliamua kuwaalika viongozi wa
nchi nyingine 35.
Shcharansky alishtakiwa kwa uhaini, hususan
kwa kupokea msaada wa fedha kutoka CIA ili kuanzisha machafuko nchini Urusi.
Baada ya mwenendo wa mashtaka, akahukumiwa kifungo cha miaka 14 jela. Baadaye akaachiliwa
huru Februari 1986, baada ya yeye na wafungwa wengine wane walipobadilishana na
majasusi wanne wa Urusi waliokuwa wamefungwa huko Magharibi. Hiki kilikuwa ni
kipindi cha utawala wa Mikhail Gorbachev ambaye wakati anaingia madarakani
mwaka 1985, aliahidi kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ili kupoza hali ya
hewa nchini Urusi. Pamoja na hali hiyo, wanachama wa kundi la Helsinki na
vikundi vingine waliendelea kudai uhuru na demokrasia na haki za binadamu hadi
Muungano wa Urusi ulipovunjika mwaka 1991.
Jun 1, 1941:
WAJERUMANI WATWAA MJI WA CRETE 1941
Tarehe kama ya leo mwaka 1941 wakati wa Vita
Kuu ya Pili ya Dunia, mji wa Crete, ambao ulikuwa ngome ya Majeshi ya Washirika
nchini Ugiriki, unatwaliwa na Wajerumani katika mapambano makali.
Mwisho mwa mwaka 1940, jeshi la Ugiriki,
likisaidiwa na jeshi la anga la Uingereza, lilifanikiwa kuizuia Italia isivamie
nchi hiyo. Lakini Aprili 1941, ushindi huo ukawa kipigo wakati kiongozi wa
Nazi, Adolf Hitler alipoliongoza jeshi lake ambalo halikuwa limepigwa ili
kuishambulia Ugiriki. Jeshi la Ujerumani lilikwenda haraka na kuishambulia Ugiriki
kiasi kwamba Waingereza waliahirisha
mpango wao wa kutuma vikosi vyao kuisaidia Ugiriki.
Aprili 23, mfalme wa Ugiriki na serikali yake
walihamia Crete, kisiwa kilichoko kusini mwa Ugiriki, na Aprili 24 vikosi vya
Majeshi ya Washirika vilihamia kisiwani humo. Wajerumani walishambulia meli
hizo na kuua askari na mabaharia 15,000 wa vikosi vya Washirika. Hadi kufikia Aprili
29, askari 50,000 wa Uingereza, Ugiriki, Australia na New Zealand walikuwa
wametua kisiwani humo.
Wiki tatu baadaye Wajerumani walianzia
harakati za kuivamia Crete, na zaidi askari 20,000 wa miavuli wa Ujerumani
walikuwa wametua kisiwani humo. Pamoja na mapambano makali, Wajerumani
walifanikiwa kuutwaa mji huo na kufikia Juni 1, askari 20,000 waliosalia wa
Vikosi vya Washirika walikuwa wametoroka.
Jun 1, 1900:
HOOVER ATEKWA KATIKA MACHAFUKO CHINA
Tarehe kama
ya leo mwaka 1900, Herbert
Hoover ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa Marekani, pamoja na mkewe Lou walikamatwa
katikati ya machafuko nchini China maarufu kama Boxer Rebellion.
Baada ya kufunga ndoa mjini Monterey,
California, mnamo Februari
10, 1899, Herbert na Lou Hoover waliondoka kwenda fungate nchini China, ambako Hoover
alitarajiwa kuanza kazi mpya kama mshauri wa uchimbaji madini kwa mtawala wa
China akiwa na kampuni ya Bewick, Moreing and Co. Wanandoa hao walikuwa wameoana
katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja wakati kundi la wanaharakati la China
lilipoasi dhidi ya wakoloni, wakwawakamata Wazungu 800 kwenye mji wa Tientsin.
Hoover aliwaongoza wazungu wenzake kujenga kingo katika makazi yao ya mji huo
wakati mkewe Lou alikuwa akisaidia katika hospitali. Inaelezwa kwamba, wakati
wa machafuko hayo yaliyodumu kwa mwezi mmoja, Hoover aliwaokoa watoto wa
Kichina katikati ya mapigano.
Baada ya vikosi vya majeshi ya
ushiriki kuwaokoa akina Hoover na kuwasafirisha wazungu wengine nje ya China,
Herbert Hoover akawa mmoja wa wamiliki wa Bewick, Moreing and Co. alikuwa
waziri wa biashara chini ya marais Warren Harding na Calvin Coolidge kuanzia
mwaka 1921 hadi 1924. Akawania urais mwaka 1928 na kushinda.
Jun 1, 1871:
JOHN WESLEY HARDIN AWASILI ABILENE
Tarehe kama ya leo mwaka 1871, John
Wesley Hardin, mmoja wa wahalifu wakubwa katika historia ya Marekani, aliwasili
huko Abilene, Kansas, ambako
alijenga urafiki wa muda na Marshal Wild Bill Hickok.
Hardin alianza tabia ya fujo na
ugomvi tangu akiwa mdogo. Wakati akiwa na miaka 14, nusura amuue kijana mmoja
wakati wakigombea msichana, akimchoma mara mbili kwa kisu. Mwaka mmoja baadaye
akamuua mwanamume mwenye asili ya Kiafrika wakati walipopambana katika mieleka.
Wakati anakwenda kufungwa jela mwaka 1878, Hardin alidai kwamba alikuwa amewaua
watu 44.
Mwaka 1871, wakati Hardin akiwa na
miaka 18, mmiliki mmoja wa ranchi wa Texas akamwajiri kijana huyo
kuongoza kundi la ng’ombe kutoka Chisholm Trail kwenda Abilene, Texas. Hardin alikuwa
anatamani kuondoka Texas, kwani siku chache kabla, alikuwa amemuua polisi wa
Texas aliyekuwa akimsafirisha yeye kumpeleka Waco kusikiliza kesi yake. Hardin alitaka
aishi maisha ya kujificha, lakini akashindwa kuzidhibiti hasira zake kwa muda
mrefu. Wakati akiswaga ng’ombe, kundi la ng’ombe wa jamaa mmoja wa Mexico
likachanganyika na ng’ombe aliokuwa nao Hardin. Alipolalamika kwa Mexico
aliyekuwa akiswaga ng’ombe hao, wakashindwa kuelewana, hivyo akaamua kumpiga
risasi ya kwenye moyo.
Wakati Hardin alipowasili Abilene,
Kansas, siku kama ya leo mwaka 1871, kiongozi wa mji huo, Wild Bill Hickok, hakuwa
na haja ya kumshtaki mtu aliyeua nje ya himaya yake. Badala yake akawa
amempenda kijana huyo ambaye alikuwa amemzidi miaka 16 na wakawa marafiki, japo
urafiki wenyewe ulikuwa wa mashaka. Kama ilivyokuwa kwa wanasheria wa magharibi,
Wildd Bill Hickok alikuwa amefanya mauaji kadhaa. Lazima alikuwa ameona kitu
ndani ya Hardin ambacho kilimvutia, akiamini kwamba kwa tabia yake ya hasira
angeweza kumtumia. Kwa upande wake, Hardin alifurahi kuwa rafiki wa mtu huyo
maarufu kwa upigaji bunduki.
Kwa wiki kadhaa, Hickok na Hardin walikunywa
pamoja na walichangia wasichana, lakini imani ya Hickok kwa kijana huyo ilikuwa
ndogo. Wakati akiwa Abilene, Hardin alikodi chumba katika hoteli ya Amerina
House. Usiku mmoja, mgeni mmoja wa chumba cha jirani alikuwa anakoroma sana. Hardin
alikerwa mno na kitendo hicho hivyo akaanza kufyatua risasi ili kumnyamazisha. Risasi
ya kwanza ilimshtua mgeni huyo, lakini ile ya pili ilimnyamazisha moja kwa
moja.
Hardin akabaini kwamba urafiki wake
na Hickok wala usingemsaidia. "Niliamini," Hardin alisema baadaye,
"kwamba kama Wild Bill angenikuta katika hali nisiyo na msaada, wala
asingesikiliza maelezo, bali angeniua ili aongeze kwenye orodha yake." Akiwa
amevaa singland, Hardin alitoroka kupitia dirisha la hoteli na kuingia mitaani.
Usiku huo akajificha kwenye jumba la kufugia farasa, alfajiri na mapema akaiba
farasi mmoja na kwenda kwenye kambi ya ng’ombe. Siku iliyofuata akaelekea
Texas, hakurudi tena Abilene.
Alikufa mwaka 1895 baada ya kupigwa
risasi mgongoni na polisi wa El Paso. Alikuwa na miaka 42.
No comments:
Post a Comment