GEORGE MIKAN AFARIKI DUNIA
Mnamo Juni 1, 2005, mchezaji mkongwe wa mpira wa kikapu aliyekuwa kwenye Orodha ya Wakongwe wa mchezo huo (Hall of Fame), George Mikan, alifariki dunia akiwa na miaka 80. Kivutio halisi cha mchezo wa kikapu wa kulipwa, Mikan aliwavutia mashabiki wengi kwenye mechi za NBA katika kipindi ambacho ligi ya mchezo huo haikuwa na uhakika kama ingeweza kushamiri.
George Lawrence Mikan alizaliwa Juni 18, 1924, mjini Joliet, Illinois, na alikuwa na urefu wa futi 6 na inchi 8 wakati anamaliza shule. Alijiunga na Chuo Kikuu cha DePaul, ambako kocha Ray Meyer alifanya kazi ya ziada kumbadili ‘ngongoti’ huyo kuwa nyota. Alimhamasisha Mikan kujenga stamina yake na kuruka kamba ili awe mwepesi. Akiwa chini ya Meyer, Mikan alibadilika na kuwa mchezaji asiyezuiliwa ndani ya DePaul, ambako alikuwa akiharibu muvu za wachezaji wa timu pinzani kiasi kwamba mwaka 1944 NCAA ikaamua kuweka sheria ya kudhibiti “ugolikipa”. Mwaka 1945, Mikan aliiongoza DePaul kupata ushindi dhidi ya Bowling Green na kutwaa taji la NIT na akatangazwa kuwa Mchezaji Mwenye Thamani Kubwa wa mashindano hayo.
Baada ya kumaliza chuo, Mikan alikwenda kucheza Ligi ya Taifa ya Basketball (NBL) akiwa na klabu ya Chicago Gears, ambayo aliiongoza ikatwaa ubingwa wa NBL mwaka 1947. Pamoja na urefu wake wa futi 6 na inchi 10 bado aliendelea kuwa mchezaji mahiri zaidi wa kikapu nchini humo. Alichezea klabu ya Minneapolis Lakers mpaka ligi ya kikapu ilipoanza kuitwa NBA.
Mwaka 1950, shirika la habari la Associated Press lilimtangaza Mikan kama mchezaji bora wa kikapu wa nusu karne ya 20.
HELEN KELLER AFARIKI
Mnamo Juni 1, 1968, Helen
Keller, mwandishi na mwalimu aliyekuwa kipofu na kiziwi tangu utoto, alifariki
dunia akiwa na miaka 87. Ulemavu wa macho na kutokusikia haukuweza kumzuia
Keller kuwa mwandishi maarufu ulimwenguni.
Helen Adams Keller alizaliwa
Juni 27, 1880, katika shamba karibu na Tuscumbia, Alabama. Akiwa mtoto alipata
ugonjwa wa scarlet fever akiwa na miezi
19 tu, ambao ukamfanya kuwa kipofu na kiziwi. Kwa miaka minne aliishi nyumbani
tu. Elimu maalum kwa vipofu na viziwi ndiyo kwanza ilikuwa inaanza wakati huo,
na ilikuwa hadi alipofikisha miaka sita ndipo wazazi wake wakampeleka kwa
daktari bingwa wa macho. Daktari huyo akawaambia wazazi wa Keller wakamuone Alexander Graham Bell, mvumbuzi wa simu na muasisi wa kufundisha
lugha za alama kwa vipofu. Bell akamchunguza Helen na akaweka utaratibu wa kuwa
na mwalimu ambaye atakuwa anakwenda nyumbani kwa akina Keller akitokea Taasisi
ya Vipofu ya Perkins mjini Boston.
Mwalimu huyo, Anne Sullivan aliyekuwa na miaka 20, naye alikuwa
na uone hafifu, lakini alikuwa amepewambinu za kufundisha vipofu.
Keller aliendelea kufanya
vizuri katika elimu yake na kupelekwa katika shule mbalimbali za wenye ulemavu
wa macho mpaka akamalicha chuo cha Cambridge huko Massachusetts.
Mwaka 1900, akakubaliwa kujiunga na chuo cha Radcliffe, kikiwa chini ya kitivo
cha Chuo Kikuu cha Harvard. Akiwa kwenye chuo hicho ndipo alipotoa kitabu chake
cha kwanza cha The Story of My Life, ambacho kilichapishwa mfululizo kwenye jarida
la The Ladies Home na baadaye kitabu kamili.
Baada ya kumaliza chuo, Keller akawa mwandishi mahiri na kutoa
vitabu kama The World I Live In (1908), Out of the Dark (1913), My Religion (1927), Helen Keller's Journal (1938), na Teacher (1955). Mwaka 1913, akaanza kufundisha
kwa msaada wa mfasiri, mwanzoni kwa niaba ya American Foundation for the Blind.
Kazi zake nzuri kwa niaba ya viziwi zilimfanya katunukiwa nishani ya Presidential
Medal of Freedom, ambayo ni nishani ya juu zaidi kwa taifa hilo kwa watu wa
kawaida, na alitunukiwa na Rais Lyndon B. Johnson.
Moderator anasema: Tutumie picha na maelezo kwa ajili ya kumbukumbu za wapendwa wetu, nasi tutazitundika mtandaoni bure bilashi.
No comments:
Post a Comment