Jun 3, 1989:
Katika ajali mbaya ya kutisha, bomba la gesi asilia linalipuka tarehe kama ya leo mwaka 1989 katika eneo la Milima ya Ural huko Russia wakati treni mbili zikiwa zinapita hapo.
Mlipuko huko mkubwa ulitokea karibu na mji wa Ufa katika iliyokuwa Muungano wa Jamhuri za Kisovieti (USSR) ambao ulitokana na maamuzi mabovu ya wafanyakazi wa bomba hilo.
Wafanyakazi hao walikuwa wanatambua kwamba presha kwenye bomba ilikuwa imeshuka siku hiyo ya Juni 3 – dalili kwamba kulikuwa na tundu mahali. Hata hivyo, badala ya kufuata taratibu za msingi na kutazama matundu, wao wakaongeza presha na kufungulia gesi kwa wingi ili kuiongeza presha iwe juu. Gesi hiyo ikaendelea kutoka (kuvuja) na kusambaa kwenye eneo la jirani, nyingi ikituama kwenye eneo la chini jirani na njia treni takriban maili moja kutoka kwenye bomba.
Wakati haya yakitokea, treni mbili zilikuwa zinakaribia kwenye Reli ya Trans-Siberia, zikipishana karibu na ilipo gesi hiyo asilia.
Ghafla gesi ikapata moto na kusababisha mlipuko mkubwa uliosambaa kwenye eneo la urefu wa maili moja. Nguvu ya mlipuko huo ikayadondosha mabehewa kadhaa ya treni yaliyoanguka nje ya reli. Mamia ya miti katika msitu wa jirani yakateketea kutokana na joto kali.
Mlipuko huo na kuanguka kwa mabehewa ya treni vikasababisha maafa makubwa kwenye treni. Zaidi ya watu 500 wakapoteza maisha yao (idadi halisi haikuweza kupatikana) na wengine wengi wakaungua na kupata majeraha makubwa. Helikopta zikapelekwa kuwabeba majeruhi na kuwakimbiza haraka hospitali.
Jun 3, 1800:
RAIS ADAMS AINGIA KATIKA MAKAO MAKUU MAPYA
John Adams, rais wa pili wa Marekani,
anakuwa rais wa kwanza kuishi Washington, D.C., wakati
alipoanza kuishi Union Tavern huko Georgetown tarehe kama ya leo mwaka 1800.
Jiji la Washington liliandaliwa kuchukuwa
nafasi ya Philadelphia kama makao makuu ya nchi katikati ya jamhuri hiyo mpya. Majimbo
ya Maryland na Virginia yalirundika udongo
pembezoni mwa Mto Potomac kuanzisha Wilaya ya Columbia, na kazi ilianza huko Washington
mwaka 1791. Mtaalamu wa majengo wa Kifaransa Charles L'Enfant alichora ramani
ya jiji hilo, likiwa na makumi ya miduara, mitaa inayokatiza, pamoja na bustani
nyingi. Mwaka 1792, kazi ilianza katika majengo ya White House katika mtaa wa 1600
Pennsylvania Avenue chini
ya usimamizi wa mtaalamu wa majengo Mmarekani mwenye asili ya Ireland James
Hoban, ambaye ubinifu wake wa Ikulu ya White House ulitokana na muundo wa Leinster
House ya jijini Dublin na mchoro wa jengo kama ulivyoelezwa katika kitabu cha
ramani cha James Gibbs (Book of Architecture). Katika mwaka uliofuata,
Benjamin Latrobe akaanza ujenzi katika majengo mengine muhimu ya serrikali, likiwemo
la U.S. Capitol.
Juni 3, 1800, Rais Adams akahamia kwenye
makazi ya muda kwenye makao makuu mapya wakati ujenzi ulipomalizika kwenye
hekalu la rais. Mnamo Novemba 1, rais alikaribishwa ndani ya White House. Siku iliyofuata,
Adams akamwandikia mkewe kuhusu nyumba yao mpya: "Naomba mbingu zilete Baraka
nzuri kwenye nyumba hii, na kwa wale wote watakaokuja kuishi baadaye. Watu wenye
busara tu ndio wanaopaswa kutawala chini ya dari ya nyumba hii!" Baadaye, Abigail Adams aliwasiki
kwenye White House, na Novemba 17 Bunge la Congress la Marekani lilikutana kwa
mara ya kwanza kwenye Makao Makuu ya Marekani.
Wakati wa Vita vya mwaka 1812, majengo yote
yaliteketezwa na wanajeshi wa Uingereza mwaka 1814 katika kulipiza kisasi cha
kuunguzwa kwa majengo ya serikali nchini Canada na majeshi ya Marekani. Ingawa mvua
kubwa ililiokoa Jengo la Capitol ambalo lilikuwa halijakamilika, lakini White
House iliteketea yote.
Hekalu hiyo lilijengwa upya na kutanuliwa kwa
maelekezo ya James Hoban.
Jun 3, 1989:
MASHAMBILIAI YA TIANANMEN YAANZA CHINA
Huku machafuko
ya kudai mabadiliko ya kidemokrasia yakiingia wiki ya 17, tarehe kama ya leo
mwaka 1989 serikali ya China inaruhusu askari wake na mizinga kushambulia eneo
la Tiananmen Square jijini Beijing kwa gharama zozote. Hadi kufikia usiku wa
manane Juni 4, majeshi ya China yalikuwa yamesafisha eneo hilo, yakiua mamia ya
waandamanaji na maelfu kukamatwa.
Mnamo Aprili
15, kifo cha Hu Yaobang, kiongozi wa zamani wa chama cha Communist (CP) ambaye
alikuwa anaunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia, kiliwaamsha wanafunzi 100,000
walioamua kukusanyika hapo Tiananmen Square kumkumbuka kiongozi huyo na kueleza
malalamiko yao kwa serikali.
Aprili
22, kumbukumbu rasmi ya Hu Yaobang ilifanyika kwenye Ukumbi wa Great Hall of
the People, na wawakilishi wa wanafunzi walibeba ujumbe hadi kwenye ngazi za
ukumbi huo, wakitaka kukutana na Waziri Mkuu Li Peng. Serikali ya China iligoma
kukutana nao, na kusababisha mgomo wa masomo katika vyuo vyote vya China na
kuitisha maandamano ya nchi nzima.
Wakipuuza
onyo la serikali la kutawanyika na kutoandamana, wanafunzi kutoka zaidi ya vyuo
vikuu 40 wakaanza kuandamana hapo Tiananmen Aprili 27. Wanafunzi hao waliungwa
mkono na wafanyakazi, wanataaluma, na watumishi wa umma, na hadi kufikia mwezi
Mei zaidi ya watu milioni moja walikuwa wamejaa kwenye eneo hilo, eneo ambalo
Mao Zedong alilitumia kuitangaza Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949.
Mnamo Mei
20, serikali ikatangaza hali ya hatari jijini Beijing, na wanajeshi pamoja na
magari ya mizinga wakaitwa kuwatawanya watu hao. Hata hivyo, umati mkubwa wa
wanafunzi na wananchi wengi wakawazuia wanajeshi hao kusonga mbele, na hadi
kufikia Mei 23 majeshi ya serikali yalikuwa yamerudi nyuma nje ya Beijing. Juni
3, huku usuluhishi wa kumaliza mgomo huo ukiwa umeshindwa kufikiwa na madai ya
mabadiliko ya kidemokrasia yakiendelea kushika kasi, majeshi yakapokea amri
kutoka serikali ya China kuivamia Tiananmen Square na mitaa yote ya Beijing.
Jun 3, 1916:
RAIS WOODROW WILSON ASAINI SHERIA YA ULINZI WA TAIFA
Mnamo Juni
3, 1916, Rais wa Marekani Woodrow Wilson anasaini sheria ya Ulinzi (National
Defense Act), ambayo ilitanua ukubwa na muundo wa ‘National Guard’—mtandao wa
vikosi vya ulinzi vya taifa ambao ulikuwa unakua kwa kasi tangu nyakati za
ukoloni.
Ingawa Theodore
Roosevelt na wanachama wengine wa Republican walikuwa wakiisukuma Marekani
iingie kwenye Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, lakini Wilson, aliyeingia madarakani
mwaka 1912, alishikiria msimamo wake wa kutofungamana na upande wowote katika
miaka kadhaa ya vita hivyo. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 1916, huku vikosi
vya Jeshi la Marekani pamoja na National Guard vikiitwa kupambana na kiongozi
wa waasi wa Mexico Pancho Villa wakati aliposhambulia majimbo ya Kusini
Magharibi ma Marekani, Wilson na Baraza la Congress wakaona kuna umuhimu wa
kuimarisha majeshi na kuongeza matayarisho ya kijeshi ya Marekani. Ndipo akasaini
sheria hiyo Juni 3.
Pia mwezi
Juni 1916, Wilson alifanikiwa kupitisha sheria ya jeshi la majini, Naval
Appropriations Act, ambayo ililenga kulifanya Jeshi la Maji la Marekani kuwa
sawa na lile la Uingereza hadi kufikia mwaka 1925. Mwezi Novemba mwaka huo,
Wilson akachaguliwa tena huku kauli mbiu ya kampeni zake ikiwa ‘Hakutuhusisha
kwenye vita’.
Jun 3, 1940:
WAJERUMANI WAISHAMBULIA PARIS KWA MABOMU
Tarehe kama
ya leo mwaka 1940, vikosi vya jeshi la anga la Ujerumani vinaishambulia Paris
kwa mabomu, na kuua watu 254, wengi wao wakiwa raia wa kawaida. Hii ilikuwa ni
wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Wakiwa wamedhamiria
kuvuruga uchumi na jeshi la Ufaransa, kupunguza idadi ya watu, na kuvunja
morali na uwezo wa kuunga mkono mataifa mengi, Wajerumani waliushambulia mji wa
Paris bila kujali watakaokufa ni raia wa kawaida, wakiwemo watoto wadogo.
Mashambulizi
hayo yalifanikiwa kuleta hofu, kwani waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa
aliweza kuwazuia maofisa wa serikali wasitoroke Paris akiwatishia kwamba
wangepata adhabu kali.
Jun 3, 1970:
NIXON ASEMA OPERESHENI YA CAMBODIA ILIKUWA NA MAFANIKIO
Katika
hotuba yake iliyoonyeshwa kwenye luninga tarehe kama ya leo mwaka 1970, Rais Richard Nixon anakiri kwamba operesheni ya majeshi ya
pamoja kati ya Marekani Vietnam Kusini iliyofanyika nchini Cambodia “ilikuwa na
mafanikio makubwa zaidi katika vita hiyo ya muda mrefu," na
kwamba alikuwa na uwezo wa kuanza kuondoa vikosi vya Marekani Kusini mwa
Vietnam.
Marekani
na vikosi vya jeshi la Vietnam Kusini walikuwa wameanzisha mapambano huko
Cambodia kuanzia Aprili 29, 1967, operesheni ambayo ilihusisha maeneo 13 ya
kuwafagia wanajeshi wa Vietnam Kaskazini umbali wa maili katikati ya Cambodia. Wanajeshi
50,000 wa Vietnam Kusini na wanajeshi 30,000 wa Marekani walihusika kwenye
operesheni hiyo ikiwa ni operesheni kubwa zaidi kufanyika mwaka huo wa 1967.
Jun 3, 1990:
BUSH NA GORBACHEV WAMALIZA MKUTANO WA PILI
Rais George Bush wa Marekani na Rais Mikhail
Gorbachev wa Urusi wamaliza mkutano wao wa siku tatu tarehe kama ya leo mwaka
1990 kwa maneno mazuri ya urafiki lakini bila kuwa na maafikiano sahihi ya
muungano wa Ujerumani.
Bush na Gorbachev walifanya mkutano wao wa
pili jijini Washington,
D.C. Mada kubwa ilikuwa hali ya baadaye ya Ujerumani
iliyoungana. Utawala wa Kikomunisti Ujerumani Mashariki ulikuwa umeanguka na
Ukuta wa Berlin ulikuwa umeporomoshwa mwaka 1989. Tofauti zikajitokeza baina ya
Marekani na Urusi kuhusu suala la Ujerumani iliyoungana katika Vita Baridi
Ulaya.
Marekani ilitaka Ujerumani mpya iwe
mwanachama wa NATO (North Atlantic Treaty Organization), umoja uliokuwa umeundwa
tangu mwaka 1949 kwa ajili ya kujihami dhidi ya Urusi iliyokuwa inataka
kujitanua Ulaya Magharibi.
Urusi nayo ikiwa tayari inahofia Ujerumani
iliyoungana na yenye nguvu za kijeshi, ikahofia Ujerumani isijiunge na NATO. Gorbachev
alipendekeza kwamba Ujerumani mpya iwe mwanachama wa NATO na Warsaw Pact, umoja
wa kikomunisti uliofanana na NATO.
Mbali ya mazungumzo ya suala hilo mkutano huo
wa pili ulizungumzia hatma ya Lithuania, jamhuri ya Kisovieti ambayo ilikuwa
imetangaza uhuru wake mwisho mwa mwaka 1989. Serikali ya Urusi iliitikia kwa
ukali kuhusu harakati za uhuru wa Lithuania, ikiweka vikwazo vya kiuchumi na
kutishi kuivamia kijeshi. Utawala wa Bush uliunga mkono uhuru wa Lithuania na
kuitaka Urusi iachane na vitisho hivyo dhidi ya taifa hilo. Hakuna maafikiano
yaliyofikiwa kwa mada zote mbili.
Jun 3, 1937:
DUKE WA WINDSOR AFUNGA NDOA
Nchini Ufaransa, tarehe kama ya leo mwaka
1937, Duke wa Windsor—ambaye alikuwa Mfalme Edward VIII wa Uingereza na Ireland
Kaskazini – anamuoa Wallis Warfield, mtalaka wa Kimarekani ambaye alisababisha
aliachie taji lake la Ufalme wa Uingereza Desemba 1936.
Edward, aliyezaliwa mwaka 1896, alikuwa mtoto
wa kwanza wa Mfalme George V, ambaye alitawala Uingereza kuanzia mwaka mwaka 1910.
Alikuwa ofisa wa jeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na katika miaka ya
1920 alifanya ziara nyingi za kiutu ng’ambo akiwa Prince wa Wales, taji
linalotolewa kwa watoto wa kiume ambao ndio wanaotarajiwa kuwa warithi wa
Ufalme wa Uingereza.
Wakati wa kushuka wa kuchumi, alisaidia
kuandaa program za kazi kwa ajili ya watu wasio na ajira na alikuwa
anaheshimiwa na watu wengi katika miaka ya mwisho ya uhai wa baba yake.
Edward, akiwa bado hajaoa wakati akikaribia
kutimiza miaka 40, akajiunga na jumuiya ya watanashati wa London na kila wakati
akawa anahudhuria pale Fort Belvedere, nyumbani kwao. Hadi kufikia mwaka 1934, alikuwa
amezama kwenye penzi zito na mwanamke Mmarekani Wallis Warfield Simpson, ambaye
alikuwa ameolewa na Ernest Simpson, mfanyabiashara Mwingireza-Mmarekani ambaye
aliishi naWallis jirani na London. Wallis, ambaye alizaliwa Pennsylvania mwaka 1896
na kukulia Maryland, awali
alikuwa ameolewa na kutalikiana na rubani wa kikosi cha jeshi la Majini la
Marekani.
Familia ya kifalme ilipinga uamuzi wa Edward
kumuoa kimada huyo aliyeolewa akaachika, lakini kufikia mwaka 1936 Edward
akaamua kumuoa Wallis. Kabla hajajadiliana uamuzi huo na baba yake, Mfalme
George V akafariki dunia Januari 20, 1936, na Edward akatawazwa mfalme.
Mfamle mpya alikuwa maarufu kwa watu wake, na
sherehe za kutawazwa kwake zilipangwa kufanyika Mei 1937. Uhusiano wake na
Wallis ukaripotiwa na magazeti ya Marekani na bara zima la Ulaya, lakini
kutokana na makubaliano ya kiungwana baina ya serikali na vyombo ya habari vya
Uingereza, uhusiano huo haukuweza kuripotiwa kwenye magazeti ya Uingereza. Oktoba
27, 1936, Wallis akapewa hati ya awali ya talaka, akiwa na nia hasa ya kuolewa
na mfalme, hali iliyoleteleza kuwepo kwa kashfa nzito.
Kwa Kanisa la England na wanasiasa wengi wa
Uingereza, mwanamke wa Kimarekani aliyeachika mara mbili alikuwa hakubaliki
kuwa Mamlkia wa Uingereza. Winston Churchill, ambaye
wakati huo alikuwa mwanachama wa Conservative asiye na sauti kuu, alikuwa
manachama pekee kumuunga mkono Edward katika uamuzi huo.
Pamoja na vikwazo vyote dhidi yake, Edward
hakuweza kuzuiwa. Akasema kwamba Wallis hatakuwa na haki ya hadhi ama mali,
lakini Desemba 2 Waziri Mkuu Stanley Baldwin akapinga uamuzi huo kwamba haukuwa
na maana yoyote.
Siku iliyofuata, kashfa hiyo nzito ikafumuka
kwenye kurasa za mbele za magazeti ya Uingereza na ikajadiliwa hadharani kwenye
Bunge. Baada ya kutofikia muafaka wowote, mfalme akaachia taji lake Desemba 10.
Siku iliyofuata Bunge likaidhinisha uamuzi huo, na siku 325 za utawala wa Edward
VIII zikafikia kikomo.
Jioni hiyo, mfamle huyo mstaafu akazungumza
kwenye radio na kueleza: "Imekuwa vigumu kwangu kubeba mzigo wa
uwajibikaji na kuachia majukumu ya Mfalme, kama ninavyotaka kufanya, bila
msaada wa mwanamke nimpendaye."
Desemba 12, mdogo ake, Duke of York, akatangazwa
kuwa Mfalme George VI. Siku hiyo mfalme mpya akamfanya kaka yake kuwa Duke wa Windsor.
Wakati huo, Edward alikua tayari ameondoka
kwenda Austria, ambako alikuwa akiishi na rafiki zake pamoja na Wallis aliyekuwa
akiendelea kusubiria talaka yake kamili. Mwanamke huyo alipata talaka yake Mei 1937.
Juni 3, 1937 yeye na Duke wa Windsor wakafunga ndoa kwenye Kanisa la Chateau de
Cande nchini Ufaransa. Kasisi wa Kanisa la England ndiye aliyefungisha ndoa
hiyo, ambayo ilihudhuriwa na watu 16 tu.
Kwa miaka miwili iliyofuata, wawili hao
walishi Ufaransa lakini walitembelea nchi nyingine za Ulaya, ikiwemo Ujerumani
ambako Duke alienziwa na maofisa wa Kinazi Oktoba 1937 na akakutana na Adolf
Hitler.
Baada ya kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya
Dunia, Duke akakubali nafasi ya kuwa ofisa mshawishi kwa Ufaransa. Juni 1940, Ufaransa
ikaangukia mikononi mwa majeshi ya Kinazi,na Edward na Wallis wakaenda Hispania.
Katika kipindi hicho, serikali ya Kinazi
ilisuka mpango wa kumteka Edward kwa malengo ya kumrejesha kwenye taji la
Ufalme wa Uingereza ili awe kibaraka wao. George VI, kama ilivyokuwa kwa waziri
mkuu, Winston Churchill, alikuwa anapinga hatua yoyote ya amani dhidi ya
Ujerumani ya Hitler. Akiwa hajui mpango wa utekaji nyara uliosukwa na Nazi lakini
akitambua huruma ya Edward kwa Nazi kabla ya vita hivyo, Churchill akamteua
haraka Edward kuwa gavana wa Bahamas huko West Indies. Edward akaenda huko Agosti
1, 1940, akikwepa meli ya Nazi SS ambayo ilitumwa kwenda kuwateka na mkewe.
Mwaka 1945, Duke akajiuzulu nafasi hiyo, na
wawili hao wakarejea kuishi Ufaransa. Edward alikwenda mara chache sana
England, hasa kuhudhuria mazishi ya Mfalme George VI mwaka 1952 pamoja na mama
yake, Malkia Mary, mwaka 1953.
Ni mwaka 1967 ambapo Duke na mkewe walialikwa
na familia ya kifalme kuhudhuria sherehe rasmi ya kifalme, kuweka shahada
liyotolewa kwa Malkia Mary. Edward alifariki jijini Paris mwaka 1972 lakini
akazikwa Frogmore, katika eneo la Windsor Castle. Mwaka 1986, Wallis na akazikwa
pembeni yake.
Jun 3, 1965:
MNAREKANI ATEMBEA ANGANI
Juni 3, 1965 maili 120 juu ya ardhi, Meja Edward
H. White II anafungua mlango wa chombo cha Gemini 4 na kutoka nje, akiwa
mwanaanga wa kwanza Mmarekani kutembea angani.
Akiwa amefungwa na mkanda wenye urefu wa futi
25 na kudhibiti mwendo wake akitumia bunduki ya hewa ya oksijeni, White alibakia
nje ya chombo hicho kwa dakika 20.
Akiwa mtembea angani, White alikuwa
ametanguliwa na mwanaanga wa Urusi Aleksei A. Leonov, ambaye mnamo Machi 18,
1965, alikuwa binadamu wa kwanza kabisa kutembea angani.
No comments:
Post a Comment