Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 3 June 2014
JAMII YAHAMASISHA KUWEKEZA SHULE ZA KATA
Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
JAMII imetakiwa kuwekeza zaidi katika shule za kata na haswa katika kuchangia ujenzi wa maabara ili kuwawezesha wanafunzi wanaosoma katika shule hizo kuweza kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi.
Aidha wanafunzi wanaosoma katika shule za kata wanashindwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho kutokana na wao kukosa maabara za kujifunzia kwa vitendo.
Hayo yalisemwa jana na diwani wa kata ya nkoaranga Godfrey Mbise alipokuwa akikabidhi fuso nane za mchanga,matofali na saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule ya kata ya sekondari ya nkoanekoli iliyopo wilayani Arumeru.
Alisema kuwa endapo jamii itaacha ngia maswala ya elimu kama wanavyoweza kuchangia maswala ya sherehe ni wazi kuwa wanafunzi wanaosoma katika shule za kata wataweza kufanya vema ktaika masomo yao ya sayansi na hivyo kulifanya taifa kupata walimu wengi wa sayansi tofauti na sasa.
“endapo kila mtu ataguswa na moyo wa kujitolea chochote tutaweza kwa kiwango kikubwa kuwawezesha wanafuzi wanaosoma katika hizi shule za kata wafanye vizuri kwani wakipata maabara watweza kujifunza kwa vitendo badala ya kujifunza tu kwa nadharia hali ambayo inawafanya wengi kutokupata uelewa wa kutosha “aliongeza Mbise.
Aidha alieleza kuwa yeye ameguswa kujitolea vifaa hivyo ambavyo vitaweza kufikisha robo tatu ya maabara katika shule hiyo kufuatia ahadi alizotoa kwa kipindi cha kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo ya kwamba endapo watamchagua atajenga ujenzi wa shule hiyo..
“kipindi cha kampeni nilitoa ahadi za ujenzi wa shule hii na kwa kipindi hiki nimeona shule hii inakabiliwa na tatizo kubwa la maabara na hivyo hivi vifaa naamini ndani ya siku chache maabara itakuwa imekamilika na hivyo kuwafanya wanafunzi wa wajifunze kwa vItendo”alisistiza diwani.
Awali mkuu wa shule hiyo Amini Mbwambo alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na maabara ya masomo ya sayansi tangu kuanzishwa na kwamba kupitia vifaa hivyo vitasaidia ujenzi kukamilika kwa haraka na hivyo kuwafanya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo kuondokana na hadha ya kujifunza kwa nadharaia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment