Picha wa hisani ya gumzolajiji.com
Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
MFANYABIASHARA wa madini, Bennedict Gabriel, (58) ameuawa na majambazi wakati akijaribu kumsaidia mfanyakazi wa duka la kubadilishia fedha la Nothern, Monica Msuya, (47) aliyekwapuliwa mkoba wenye shilingi milioni 5.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 3:15 asubuhi mtaa wa Maeda karibu na mzunguko wa Mnara wa Saa ambapo imefahamika kuwa mfanyabiasha huyo ni mume wa diwani wa viti maalum, Lilian Mmasi, (CCM) kwenye halmashauri ya jiji la Arusha.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,Liberatus Sabas, jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo hilo lililozua gumzo kwenye maneo mbalimbali ya jiji la Arusha, ambapo alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Sabas alisema kuwa Msuya alichukua kiasi hicho cha fedha kwenye hoteli ya Impala na kuelekea nazo kwenye ofosi yake kwa kutumia gari la kukodi (tax).
"Mara baada ya kushuka na kuanza kufungua mlango wa ofisini kwake, wakati akifungua mlango ghafla alitokea kijana mmoja na kutaka kumnyang'anya mkoba wake ndipo alianza kumpambana nae.
"Lakini kijana huyo alimpiga Msuya makofi mawili na kumpiga ngwara kisha kuanguka chini, Monica alipiga kelele ya kuomba msaada huku akiwa ameshikilia mkoaba wake wenye pesa'" alisema Sabas.
Alisema kuwa marehemu Gabriel alijitokeza kumsaidia Msuya ila kijana mwingine aliyekuwa kwenye pikipiki alitoa bunduki aina ya short gun na kumlenga marehemu Gabriel na walifanikiwa kupora mkoba huo wenye fedha na kutoweka eneo hilo kwa kutumia pikipiki yao nyekundu aina ya Toyo.
Kamanda Sabas alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
Naye Mke wa marehemu Akiongea kwa njia ya simu, mke wa marehemu Gabriel, Lilian alisema kuwa katika maisha yao ya ndoa walibarikiwa kupata watoto watatu.
Allisema kuwa mume wake alikutwa na tukio hilo lililokatisha uhai wake wakati akielekea kanisani peke yake hakuwa ameongozana naye.
Diwani Mmasi alisema kuwa mazishi yamepangwa kufanyika keshokutwa (alhamisi) nyumbani kwao Kata ya Moshono karibu na shule ya sekondari ya Moshono.
Wakati huohuo Askari Polisi , E 5921 CPL Justine amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Nissan mini bus lenye namba za usajili T 319 AXT maeneo ya Ngarenaro jijini hapa.
Kamanda wa polisi, Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya 1:30 usiku wakati askari huyo alipokuwa akitembea kwa miguu ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa uya Mount Meru.
No comments:
Post a Comment