Rais wa muda
mrefu wa kampuni ya Motion Picture Association of America (MPAA), Jack Valenti
alipata kusema: “Kama Hollywood ni Mlima Olympus, basi Lew Wasserman ni Zeus
(mungu).”
Wasserman,
wakala na mtendaji mkuu wa studio anayetajwa kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa
katika Hollywood kwa miaka 40 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, alifariki Juni 3, 2002 akiwa na miaka 89.
Alizaliwa
Cleveland, Ohio, akiwa mtoto wa Wayahudi wa Orthodox waliohamia
Marekani wakitokea Russia. Alianza kuigiza mitaani akishiriki michezo
mbalimbali kabla ya kupata kazi kwenye kampuni ya Music Corporation of America
(MCA) jijini Chicago. Mwaka 1938, mwanzilishi wa MCA Jules Stein
alituma wasaidizi wake wakatanue biashara za kampuni yake huko Hollywood, Los
Angeles, na kufikia mwaka 1948 akamteua Wasserman kuwa rais wa MCA.
Wasserman
akaanza kupanua biashara ya filamu ya MCA, akiingia mikataba na nyota
mbalimbali wa Hollywood na kuwaibua wengine. Baada ya WWII, orodha ya wateja wa
MCA ilikuwa ndefu ikihusisha wachezaji filamu wakubwa, wakiwemo Bette Davis,
Errol Flynn, James Stewart, Judy Garland, Henry Fonda, Myrna Loy, Fred Astaire,
Ginger Rogers, Jack Benny, George Burns, Gracie Allen, Gregory Peck and Gene
Kelly.
Pia
Wasserman alikuwa amewaajiri waongoza filamu mahiri kama Billy Wilder na Alfred
Hitchcock.
No comments:
Post a Comment