CHARLES MUGUTA KAJEGE
Alizaliwa Juni 3, 1962. Aliingia Bungeni mwaka 2005 kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM). Baada ya matokeo kutenguliwa na Mahakama Kuu mwaka 2009
kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na Mtamwega Mgaywa wa TLP,
alikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa iliyomrejesha tena. Lakini akashindwa
kwenye kura za maoni na Alphaxard Kangi Lugola. Elimu ya msingi aliipata katika
shule ya Namibu (1968 hadi 1974), elimu ya sekondari aliipata katika shule ya
sekondari Kazima (1977 hadi 1980) baadaye akajiunga na kidato cha tano na sita
katika shule ya Azania (1981 hadi 1983). Kati ya mwaka 1986 na 1992 alihitimu
shahada ya kwanza ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Bogazigi, mwaka 1994
akahitimu stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo cha Centre For
Foreign Relations, mwaka 1997 na 1999 alihitimu shahada ya uzamili katika Fedha
na Uchumi katika Chuo Kikuu cha London, Uingereza, na mwaka 2000 na 2002
alihitimu shahada ya uzamili katika Fedha na Masoko kutoka Chuo Kikuu cha
Miami, Marekani.
Tangu mwaka 1984 hadi 2005 alikuwa Ofisa wa Mambo ya Nje katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Jun 3, 1936:
MWANDISHI LARRY MCMURTRY AZALIWA
Larry
McMurtry, mmoja wa waandishi wa kisasa wenye vipaji wa magharibi, anazaliwa
siku kama ya leo, lakini mwaka 1936 huko Wichita Falls, Texas.
Familia
ya McMurtry ilikuwa imejihusisha na masuala ya ranchi Texas kwa mizazi vitatu,
na yeye alianza kujihusisha na masuala ya ranchi tangu akiwa mdogo.
Hata
hivyo, McMurtry, alikuwa anapendelea zaidi vitabu kuliko mifugo. Baada ya
kusoma Chuo Kikuu cha Rice, McMurtry alielekea California, ambako alijiunga na
program ya uandishi wa ubunifu ya Wallace Stegner katika Chuo Kikuu cha Stanford.
Stegner,
ambaye alikuwa ameandika vitabu kadhaa vya riwaya vilivyofanya vizuri, kikiwemo
The Big Rock Candy Mountain (1943), alibaini kipaji cha McMurtry
na akamshawishi aandike kuhusiana na Magharibi ya sasa.
Akiwa
hana uhakika kama angeweza kuishi kwa kutegemea uandishi, McMurtry akaanzisha
maduka ya vitabu katika miji ya ya Texas na Washington, D.C., na
kuugawanya muda wake kati ya maeneo hayo mawili. Katika kitabu chake cha kwanza
cha riwaya, McMurtry pia alihusisha masuala ya mijini na vijijini, ikiwa ni
staili mpya.
Vitabu
vya mwanzo kabisa vya McMurtry, ni pamoja na Horseman, Pass By (1961), ambacho kilikuwa msingi wa
filamu maarufu ya Hud. Vitabu vingine vya McMurtry ni
pamoja na Leaving Cheyenne (1963), The Last Picture Show (1966), Moving On (1970), Lonesome Dove (1986), Anything for Billy (1988),
na Buffalo Girls (1990).
No comments:
Post a Comment