Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 3 June 2014

MIMBA NA SIRI YA PRECIOUS, KAMANDA YONA MARO ULIWAZA NINI HASA?!


Ndugu zangu,
Kati ya mambo ambayo kwa hakika yananifanya kila wakati niwe ninatafakari kuhusu mustakabali wa taifa letu, hasa katika mukhtadha wa sasa wa kugubikwa na wimbi la ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, ni makala hii ya kufikirisha ya Yona Fares Maro.
Ukisoma kwa haraka unaweza kusema ni porojo kama tulizozizowea, lakini kwa hakika mwandishi hapa aliacha kazi zake akafanya kazi iliyotukuka, ambayo inaeleza kwa kina kuhusu namna tunavyoweza kuwarithisha watoto wetu tabia njema ama mbaya tangu wakiwa tumboni!
Kisa na 'Mimba na Siri ya Precious' alikiandika Bwana Maro kupitia jukwaa la Wanabidii Februari 6, 2012, lakini binafsi nadhani ni dira murua kwetu sote kujadiliana na kukumbushana kila wakati ili kuhakikisha kwamba tunabadili mienedo yetu katika misingi ya utawala bora.
Mwenyewe anaweza kudhani kazi aliyoifanya ni ya kawaida tu, kama zilivyo nyingine, au amefanya kazi nyingine kubwa zaidi ya hiyo, lakini hiki ni kitu ambacho nadhani tunafaa kukirejea tena na tena.
Hebu tukiangalie kwa pamoja na tutafakari:..

From: Yona Maro <oldmo...@gmail.com>
Sent: Monday, February 6, 2012 10:41 AM
Subject: [wanabidii] Mimba na Siri ya Precious

Pregnancy
- Mimba ilitungwa baada ya baba kutoa hongo kwa kimada
- Ili kuthibitisha kama ni mimba kweli kimada akatoa rushwa kwa daktari ili apimwe harakaharaka kwa kuwa kulikuwa na msongamano wa wagonjwa
- Kila alipoenda kliniki wakati wote wa Ujauzito alitoa 'chai' ili ahudumiwe vizuri na wauguzi na madaktari
- Hata wakati wa kujifungua akatoa 'chai' kwa manesi apate huduma safi

Baada ya Kujifungua
- Baada ya kujifungua aliendelea kutoa hongo awe wa kwanza kuhudumiwa, mwanae awe wa kwanza kuchomwa sindano za Chanjo n.k.
- Mwanae akaitwa 'Precious'

Elimu kwa Precious
- Kuandikishwa chekechekea akatoa hongo ili Precious apate nafasi katika shule nzuri kwa kuwa nafasi zilikuwa chache, Precious anaangalia
- Kuandikishwa shule ya msingi mchezo uleule, Precious anaangalia
- Tena sekondari akatoa 'Chai' kwa mwalimu wa Hisabati ili Precious apate alama nzuri
- Chuo kikuu Precious hali ikawa ngumu, akagawa uroda kwa mkufunzi ili apate alama nzuri

Kazi
- Precious akagawa uroda ili apate kazi, akapata
- Precious akatishiwa mara kwa mara kufukuzwa kazi kutokana na utendaji mbovu kinga ikawa ni kugawa uroda
- Akatumia nafasi yake kwa manufaa yake binafsi
- Kwa tamaa ya vitu vya thamani kuliko mshahara wake akaendelea kupokea rushwa

Ndoa
- Kwa kuwa wazazi wake (baba yake) hakuwa mwaminifu katika ndoa yake (Precious ni mtoto wa kimada), naye Precious hakuona sababu ya kuwa mwaminifu ktk ndoa
- Watoto wake wote walifuata mlolongo kama wa kuzaliwa kwake

KIFO
- Hata alipougua ghafla , hongo ikatumika apate huduma bora lakini Mungu alimpenda zaidi
- Walipoenda kuchonga jeneza, wakakuta kuna order nyingi ikabidi watoe 'Cha Juu' ili kuchukua jeneza lilokuwepo tayari
 - Wakati wa mazishi Kwaya iliyotakiwa kuimba wakati wa Maombolezo ilikuwa na safari , ikapewa 'cha juu' ili kuahirisha safari

MWISHO
Kwaya ikaimba na Kumsifia Precious alivyokuwa 'mtumishi mwema wa Mungu', tena wakamwomba Mungu ampokee kwa mikono miwili , amuepushe na Moto wa milele.
Risala ikasomwa, na kusifia utumishi wake uliotukuka, tena kaacha pengo lisilozibika.

Take Home Message
- Wazazi 'huwapakaza' watoto wao matope ya dhambi toka pale mimba inapotungwa hata baada ya kuzaliwa
- Watoto wote huakisi tabia walizojifunza toka kwetu, kama wazazi (Observational Learning)
- Kama hatuwezi kuwa wawazi hasa pale kaburini hata kwa mtu aliyekufa na sifa mbaya akasifiwa basi tunahalalisha matendo mabaya aliyoyafanya marehemu.
- Ili Kupambana na Rushwa twahitaji kuanzia wakati wa Ujauzito, mtoto azaliwe bila rushwa, akue bila rushwa n.k
   - KWA LEO NI HAYO TU!!!

CREDIT ZA KUTOSHA KWA WANABIDII, YONA MARO IN PARTICULAR

No comments:

Post a Comment