Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 2 June 2014

'HAPPY BIRTHDAY': SERGIO AGUERO, FREDDY ADU, ABBY WAMBACH, SALLY KELLERMAN, DENNIS HAYSBERT


SERGIO AGUERO


Mshambuliaji mahiri wa Manchester City ya England na timu ya taifa ya Argentina ambaye alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1988 huko Argentina. Alijiunga na Man City mwaka 2011 baada ya kufunga mabao 74 katika mechi 175 alizoichezea Atletico Madrid ya Hispania kati ya mwaka 2006 na 2011. Alianza kuicheza timu ya taifa ya Argentina mwaka 2006. Maisha yake ya soka yalianzia katika klabu ya Independiente wakati akiwa na miaka 15 ambako alilelewa kwa miaka sita katika kikosi cha vijana. Aliisaidia Argentina kutwaa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki jijini Beijing, China mwaka 2008. Ana mtoto wa kiume aitwaye Benjamin aliyezaa na mkewe wa zamani Giannina Maradona, binti wa Diego Armando Maradona.

ABBY WAMBACH

 

Mwanasoka huyu wa kike wa Marekani alizaliwa New York tarehe kama ya leo mwaka 1980. Ni nyota mahiri wa timu ya taifa ya wanawake wa Marekani aliyojiunga nayo mwaka 2003, akaisaidia kutwaa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi mwaka 2012 akifunga mabao matano katika mechi sita na kuwa mfungaji bora wa miaka yote wa timu hiyo ya wanawake ya Marekani, akimpiku Mia Hamm. Alipata Kiatu cha Shaba na Mpira wa Fedha katika Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2011. Ana ndugu wawili wa kike, Laura na Beth Wambach.


MARTHA WASHINGTON

Sarafu iliyokuwa na picha yake. 

Mke wa Rais George Washington wa Marekani aliyezaliwa Virginia, Marekani tarehe kama ya leo mwaka 1731. Alifariki dunia Mei 22, 1802 akiwa na miaka 70. Mumewe alitumia utajiri wake (Martha) kuuchonga Mlima Vernon na kupata ardhi ya kutosha na watumwa. Kabla ya kuwa maarufu alikuwa ameolewa na mtu asiyejulikana, Daniel Parke Custis, ambaye walibahatika kupata watoto wane. George Washington alikuwa mumewe wa pili ambaye walioana Januari 1759. Aliishi miaka 20 kabla Washington hajawa rais.

DENNIS HAYSBERT

 

Mwigizaji mahiri huyu wa luninga aliyezaliwa California tarehe kama ya leo mwaka 1954. Aliigiza kama Rais wa Marekani katika tamthiliya ya 24 akiwa na Kiefer Sutherland aliyeigiza kama ‘Jack Bauer’ na pia akaigiza kama Sajini kwenye filamu ya The Unit. Anafahamika zaidi pia katika matangazo ya Allstate. Aliamua kujiunga na masomo ya uigizaji baada ya kumaliza sekondari licha ya kupewa scholarship nyingi katika michezo. Aliigiza kama mcheza baseball Pedro Cerrano katika filamu ya Major League. Alimuoa Elena Simms wakaishi kwa miaka minne kabla ya kumuoa mkewe wa pili Lynn Griffith mwaka 1989 na kutalikiana naye miaka 12 baadaye.

JOHN RANDOLPH

 

Mwanasiasa huyu wa Marekani alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1773 huko Virginia. Alikuwemo kwenye Bunge la Wawakilishi (House of Representatives) kwa vipindi kadhaa kati ya mwaka 1799 na 1833 alipofariki Mei 24 akiwa na miaka 59. Alikuwa kiongozi wa chama cha ‘Old Republicans’, ambacho kilimeguka kutoka Chama cha Democratic-Republican ambacho kilikuwa kikitetea uhuru wa majimbo.
Alisoma vyuo huko New Jersey, New York na Philadelphia. Alishindwa kipindi kimoja cha uchaguzi kutokana na kupinga Vita vya mwaka 1812 na alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa jumuiya ya American Colonization Society mwaka 1816, kuwapeleka weusi waliokuwa huru katika koloni barani Afrika. Anatokea katika familia ya Thomas Rolfe na Pocahontas na alikuwa binamu yake Rais Thomas Jefferson.


SALLY KELLERMAN

 

Mwigizaji huyu alizaliwa California tarehe kama ya leo mwaka 1937 na ametimiza miaka 76. Aliteuliwa kuwania Tuzo ya Oscar katika kitengo cha Best Supporting Actress baada ya kushiriki vyema kwenya filamu ya M*A*S*H akicheza kama Hot Lips Houlihan. Kabla ya kuwa staa alisoma katika shule ya Actors Studio West pamoja na Robert Blake na akaanza kushiriki kwenye filamu ya The Boston Strangler. Aliigiza kama Louise katika filamu ya Brewster McCloud mwaka 1970. Alifunga ndoa na Johnathan Krane mwaka 1980 na wawili hao wakawaasili watoto mapacha.

FREDDY ADU

 

Mwanandinga huyu Mghana, mzaliwa wa Australia na raia wa Marekani alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1989 na anatimiza miaka 25. Ni winga wa timu ya soka ya taifa ya Marekani ambaye ameng’ara sana na akawa mwanamichezo mdogo zaidi kusaini mkataba wa soka ya kulipwa nchini Marekani akiwa na miaka 14, na pia akawa mchezaji mdogo zaidi kushiriki katika Ligi Kuu ya Soka ya Marekani (MSL) akicheza kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 16. Alikuwa mfungaji bora katika timu ya taifa ya Marekani chini ya miaka 14 ya Program ya Maendeleo ya Olimpiki. Alichaguliwa mara mbili katika timu bora ya MSL (All-Star), mwaka 2004 na 2006. Alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki JoJo.

 

KATIE KELLY

 

Mwanasoka huyu wa kike wa Marekani leo ametimiza miaka 27. Alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1987 huko Missouri. Ni mlinzi mahiri ambaye alianza kucheza soka ya kulipwa mwaka 2010 akiwa na klabu ya Kristianstads DFF, kabla ya kuhamia F.C. Indiana mwaka 2011 na baadaye kusajiliwa na FC Kansas City mwaka 2013. Alicheza soka ya utotoni katika kituo cha St. Teresa's Academy na wakati akiwa chuo kikuu, alichezea timu ya Chuo Kikuu cha Marquette. Baba yake ni Neil na mama yake Shelley.

MODERATOR: LETENI PICHA ZENU ZA 'BIRTHDAY' TUZITUNDIKE BURE KABISA



No comments:

Post a Comment