Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 2 June 2014

MKUTANAO WA WADAU WA HUDUMA YA AFYA YA MSINGI (PHC) KWA JAMII MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa Huduma ya Afya ya Msingi (PHC – Primary Health Care) kwa Wananchi Mkoani Rukwa tarehe 30 Mei 2014 katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga. Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya msingi kuhusu afya ya jamii yalijadiliwa na kuwekewa mpango kazi wa utekelezaji katika kuimarisha afya ya jamii Mkoani Rukwa. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito, maendeleo ya shughuli za usafi wa mazingira, utekelezaji wa shughuli za chanjo ya magonjwa mbalimbali, utaratibu wa utoaji wa PF 3, hali ya homa ya Dengu na lishe. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Katika salam zake za ufunguzi alisisitiza juu ya usafi wa mazingira ambao ndio kinga kuu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza kama Dengu na magonjwa ya mlipuko. Aliupongeza mpango wa Sumbawanga Nga’ara ambao kwa kiwango kikubwa umeleta mabadiliko ya usafi katika mji wa Sumbawanga tofauti na siku za nyuma. Aliipongeza pia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa hatua waliyofikia wa kuagiza magari mawili ya kubebea taka yatakasaidia katika kuimarisha mpango huo wa usafi katika Manispaa ya Sumbwanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akiwasilisha mada ya hali ya huduma ya afya ya mama, baba na mtoto Mkoani Rukwa katika mkutano huo.
Mwanasheria Mfawaidhi wa Serikali Mkoa wa Rukwa Msomi Prosper Rwegerera akiwasilisha mada ya utaratibu wa utoaji wa PF 3 kwa mtu alijeruhiwa. Alisema PF 3 ni muhimu katika ushahidi wa kimahakama pale mtu atakapokuwa anadai haki yake mahakamani kutokana na jeraha aliliopata na pia inakuwa ni kithibitisho cha kisheria kwa kilichotokea kwa majeruhi husika. Katikati ni Afsa Afya wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Kenedy Kyauke.
Sehemu ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwa umahiri mkubwa.
Sehemu ya wadau wa mkutano huo.
Sehemu ya wadau wa mkutano huo ulioshirikisha wajumbe mbalimbali kutoka katika sekta ya afya, asasi za kidini, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa, watumishi wa Serikali na Sekta binafsi na wadau wengine waalikwa.
- Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment