Na Daniel Mbega
Ndugu zangu,
Tunaendelea na simulizi yetu ya
kufuatilia ‘Nyayo za Chifu Mkwawa’. Samahani sana kwa kutoendelea kwa siku
kadhaa zilizopita. Niko safarini na mahali nilipo wakati mwingine mtandao
unasumbua, lakini pia majukumu mengine yamenibana.
Katika sehemu iliyopita,
tuliona jinsi vita vya Lugalo vilivyoanza. Tumeona muundo wa jeshi la Mkwawa na
lile la Wajerumani. Tumeona pia jinsi mapigano hayo ya kushtukiza
yalivyowapoteza askari wengi wa Wajerumani huku wachache tu wakinusurika lakini
wakiendelea kupigania roho zao.
Hadi wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, nilimsikia Sajini Tiedemann akisema alikuwa ameumia kabla hajafyatua risasi. Haikuwa rahisi kuona zaidi ya umbali wa hatua tano msituni kutoka pale njiani. Pia hakuna ambaye aliweza kunusurika kwa sababu Wahehe walikuja kwa kasi… Ni wazi walipanga kutushambulia baada ya kufika katikati msitu. Kuvurugika kwa mipango yao kulichangiwa hasa na kitendo cha Luteni von Zitewitz kufyatua risasi…”

Muanzilishi
wa Himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki, Carl Peters, baadaye Novemba 23, 1891
alimwandikia Gavana von Soden akisema kwamba, katika mapambano mengine na
makabila mbalimbali ya Tanganyika, ilikuwa ni bahati tu kwao kutoweza kupata
madhara kama waliyopata Wajerumani pale Lugalo, kwani mafunzo yao ya vita
yalikuwa yanalenga zaidi kupigana wakiwa wamejipanga pamoja kwa mbinu maalum.
Hawakuwa wamejifunza kupigana kila mtu kwa uwezo wake, bali walitegemea zaidi
kushambulia kwa pamoja.
Iliwachukua
Wahehe dakika 15 tu (kuanzia saa 1:15 hadi 1:30 asubuhi) kuwafyeka Wajerumani
na majeshi yao. Von Zelewiski aliuawa kwa kupigwa nyundo kichwani akiwa
amepanda punda wake wakati akijiandaa kuwafyatulia risasi wapiganaji wa Mkwawa.
Kabla hajadondoka akachomwa mkuki ubavuni.
Hii
ndiyo asili hasa ya jina la ‘Nyundo’ kutokana na kamanda huyo wa Wajerumani
kuuawa kwa nyundo!
Kuhusiana
na kifo cha Kamanda von Zelewiski, kama Mjerumani Tom von Prince alivyoandika
baadaye, “Kama nilivyosimuliwa baadaye… na Wahehe walioshuhudia, alijitetea
mwenyewe kwa kutumia bastola yake kubwa na kuwapiga risasi watu watatu, wakati
kijana mmoja wa Kkihehe alipomchoma na mkuki ubavuni. Kijana huyo alikuwa na
umri wa miaka 16 tu na alizawadiwa ng’ombe watatu na Mkwawa kwa kitendo hicho.”
Luteni von Pirch na Dk. Buschow pia waliuawa wakiwa juu wa
punda wao ambapo majeraha yao yalikuwa makubwa mno. Karibu askari wote wa
Kikosi cha 7, Kikosi cha Silaha, Kikosi cha 5 na baadhi ya askari wa Kikosi cha
6 waliuawa kabla hata hawajajua wafanye nini.
Luteni von Heydebreck, Luteni Usu Wutzer na Murgan Effendi
pamoja na askari 20 hivi ndio waliofanikiwa kukimbia kutoka eneo hilo la
mapigano na kukimbilia upande mwingine wa mlima na kuweka ngome wakijilinda
dhidi ya mashambulizi ya Wahehe. Wapiganaji hao wa wajerumani walijificha
kwenye pagala moja la tembe lililokuwa limetelekezwa mlimani. Askari mmoja Msudani
ndiye aliyekiona kibanda hicho.
Lakini
von Heydebreck aliishuhudia vita hiyo katika kipindi cha dakika mbili au tatu
tu kabla ya kupoteza fahamu. “Kulingana na ushuhuda wa Wahehe walioshiriki
mapigano yale, vita hivyo havikumalizika mapema kama ambavyo Wazungu wa mstari
wa nyuma walivyotegemea, badala yake askari walionusurika waliendelea kupambana
hadi saa 4:30 asubuhi na kuwaua maadui wengi (Wahehe).”
Tutaendelea...
No comments:
Post a Comment