Mtalii ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa anawekwa kwenye machela baada ya kuzidiwa na kushindwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Vijana wakimkimbiza kwa machela mtalii aliyezidiwa mlimani ili kumshusha chini.
Kupanda Mlima Kilimanjaro ni fahari kubwa kwa sababu ndio mrefu kuliko yote Afrika. Lakini changamoto zake ni nyingi ikiwemo kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Watu wengi wanaopanda wanashindwa kufika katika kilele cha Uhuru Peak kwa sababu mbalimbali, ikiwemo masuala ya kiafya. Hii pia inatokana na kubadilika kwa hali ya hewa mlimani kadiri unavyozidi kupanda.
Hata hivyo, kupanda taratibu kutakusaidia usipate homa ya kupanda mlima na hata kuzidiwa, vinginevyo itabidi kutafuta ilipo machela ili uteremshwe chini.
Daniel Mbega
No comments:
Post a Comment