Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Katika jitihada za kuhami kituo, askari polisi walitoa tahadhali mbalimbali za kuwataka wananchi hao watawanyike ikiwemo kupiga mabomu ya machozi, lakini wananchi hao waliendelea kukaidi amri hiyo. Katika purukushani hizo za askari kutetea kituo na wavamizi kuendelea kuharibu mali za kituo ikiwemo kukichoma moto, wananchi 3 walipoteza maisha na wengine 3 walijeruhiwa.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo (CP) Paul Chagonja kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuongeza nguvu katika Operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo, ili wafikishwe katika mkondo wa sheria haraka.
Jeshi la Polisi linalaani vikali tukio hilo linaloashiria vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani, tukio ambalo limesababisha vifo na majeruhi pamoja na kujenga hofu miongoni mwa jamii.
Aidha, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro hususani wilaya ya Ulanga kata ya Malinyi, kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wakati uchunguzi ukiendelea, mtu yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao anaombwa kutoa taarifa kwenye namba ya simu ifuatayo 0754 78 55 57 au katika kituo chochote cha Polisi, ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment