Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 30 December 2013

BASI LA SUPER FEO LAUA MBELE YA TRAFIKI IRINGA





Basi la Super Feo, ambalo blog hii ilishindwa kupata namba zake za usajili mara moja, lililokuwa likitokea Songea kwenda Dar, limeua mtoto mbele ya askari wa Usalama Barabarani katika eneo la Igumbilo, mjini Iringa leo asubuhi majira ya saa 5.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo mbaya ilitokea kwa kinachoelezwa kuwa ni uzembe wa dereva ambaye alisogeza gari huku mlango ukiwa haujafungwa.
Inaelezwa kwamba, mtoto aliyeuawa papo hapo ambaye jina lake pia halikuweza kupatikana mara moja, alikuwa ni miongoni mwa abiria wa basi hilo, ambapo yeye na mwenzake walikuwa wameteremka ili kujisaidia baada ya basi hilo kusimama kwa ukaguzi wa kawaida.
Wakati mtoto huyo akitaka kupanda, dereva wa basi hilo alilisogeza mbele ambapo mlango ulimsukuma mtoto na kuingia uvunguni mwa gari na kukanyagwa kichwani.
Mashuhuda wanasema, mtoto huyo alikuwa ameongozana na mjomba wake aliyekuwa akimpeleka Dar es Salaam kwa wazazi wake ili kula sikukuu ya Mwaka Mpya.
Mtandao huu utawaletea taarifa zaidi za tukio hilo.

No comments:

Post a Comment