TAARIFA
KWA UMMA
ZABUNI
YA 4 YA KUNADI VITALU VYA
UTAFITI
WA GESI ASILIA
Utangulizi.
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
tarehe 25/10/2013 ilizindua rasmi zabuni ya nne ya vitalu vya utafiti wa mafuta
na gesi asilia vilivyoko bahari kuu na Ziwa Tanganyika kaskazini. Uzinduzi wa
zabuni hii ulihusisha vitalu 7 vilivyoko bahari kuu (deep offshore blocks)
pamoja na kitalu cha Ziwa Tanganyika kaskazini (Lake Tanganyika North).
Vitalu vya bahari kuu vipo katika kina cha maji kati ya mita 2000 na 3000 wakati kitalu cha Ziwa Tanganyika kinafikia kina cha mita 1500. Mchakato wa zabuni utafungwa rasmi baada ya miezi sita na Zabuni zitakazowasilishwa kabla ya saa nne asubuhi ya Alhamisi ya tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2014. Zabuni zitafunguliwa kwa uwazi mbele ya washiriki wa mnada watakaopenda kuwepo ama kuwakilishwa siku ya ufunguzi.
Vitalu vya bahari kuu vipo katika kina cha maji kati ya mita 2000 na 3000 wakati kitalu cha Ziwa Tanganyika kinafikia kina cha mita 1500. Mchakato wa zabuni utafungwa rasmi baada ya miezi sita na Zabuni zitakazowasilishwa kabla ya saa nne asubuhi ya Alhamisi ya tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2014. Zabuni zitafunguliwa kwa uwazi mbele ya washiriki wa mnada watakaopenda kuwepo ama kuwakilishwa siku ya ufunguzi.
Majina ya vitalu vinavyonadiwa ni kama inavyooneka
katika jedwali hapa chini.
Nambari
|
Jina la kitalu
|
Eneo (mita za Mraba)
|
1
|
Block 4/2A
|
3630
|
2
|
Block 4/3A
|
2620.3
|
3
|
Block 4/3B
|
3045.0
|
4
|
Block 4/4A
|
2963.3
|
5
|
Block 4/4B
|
3048.9
|
6
|
Block 4/5A
|
2545.3
|
7
|
Block 4/5B
|
3052.6
|
8
|
Lake Tanganyika North
|
9670.2
|
Faida za Ugawaji wa Vitalu vya utafiti kwa
njia ya Zabuni
Utaratibu huu wa kutoa maeneo kwa kutumia zabuni
hutumika sehemu nyingi duniani zikiwemo nchi nyingi za Bara la Afrika
(Msumbiji, Kenya, Libya, Togo, Misri, Sudan, Senegal, Somalia nk.), Asia
(China, Oman, Malaysia, Indonesia, Qatar, Bahrain nk), Ulaya (Georgia, Nepal,
Guyana nk.), Amerika (kusini na kaskazini). Umuhimu wa kugawa vitalu kwa njia
ya zabuni ni pamoja na:
· kuhakikisha kuwa mchakato mzima unafanyika
kwa njia ya uwazi;
2
·
kutoa vitalu kwa utaratibu mzuri ili kuweza
kuendeleza rasilimali kwa gharama nafuu endapo ugunduzi utafanyika;
·
kupata wawekezaji bora wenye mitaji,
utaalamu na uzoefu wa kufanya utafutaji;
·
kutoa nafasi kwa wawekezaji wazalendo
kushiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi; na
·
kutoa fursa kwa makampuni mengi na wataalamu
mbalimbali kuona takwimu (data) zilizopo na hivyo kupata kwa wingi maoni
mbali mbali ya kitaalamu kuhusiana na uwezekano wa kuwepo mafuta na/au gesi.
Gharama za kushiriki
kwenye Zabuni
Gharama za kushiriki kwenye
zabuni zinajumuisha ada isiyorejeshwa ya ushiriki kwenye zabuni, gharama za
kununulia kifurushi cha zabuni yenyewe, gharama za kununulia vifurushi vya data
za mitetemo cha lazima kwa waomba zabuni wa vitalu zilivyopo bahari kuu na Ziwa
Tanganyika kaskazini na gharama za kununulia „data‟ za nyongeza za hiari kadri mshiriki atakavyoona inafaa.
Ada
ya ushiriki kwenye zabuni isiyorejeshwa ambayo ni Dola za Marekani 50,000.
Gharama halisi ni kama zilivyonyambuliwa hapa chini:
Gharama kwa muombaji
wa vitalu vya baharini
i.
Gharama za kununulia kifurushi cha lazima
cha zabuni za vitalu vya bahari kuu (Bidding Round Data Package (BRDP) for
deep offshore blocks) ni Dola za Marekani 750,000 kwa kila kifurushi.
ii.
Gharama za kununulia kifurushi cha lazima
cha taarifa za mitetemo ya „Mandatory 2D SPAN‟ ni Dola za Marekani milioni 3.375 kwa kila
kifurushi.
iii.
Gharama
za kununulia taarifa za hiari za mitetemo ya „Optional 2D
SPAN data‟ ni Dola za Marekani 750 kwa
kila kilomita moja ya urefu.
Gharama kwa muombaji wa kitalu cha kaskazini
ya Ziwa Tanganyika
i.
Gharama za kununulia kifurushi cha lazima
cha zabuni ya kitalu cha Ziwa Tanganyika kaskazini (BRDP for Lake Tanganyika
North) ni Dola za Marekani 350,000 kwa kila kifurushi.
ii.
Gharama za kununulia taarifa za hiari za
mitetemo ya „Optional
Phase
I and Phase
II data‟ ni Dola
za Marekani 220
kwa kila
kilomita moja ya urefu.
Waomba zabuni ni lazima
waoneshe ushahidi wa kununua taarifa (data) kwa kuambatisha stakabadhi ya
ununuzi pamoja na mkataba wa kutunza siri waliosaini katika zabuni
watakazorejesha.
Kabla ya kushiriki katika
uombaji zabuni, makampuni yote ni lazima yaweze kutimiza masharti ya zabuni
yaliyowekwa. Makampuni inabidi yanunue kifurushi cha zabuni husika (Bid
Round Data Package – BRDP).
Kifurushi cha zabuni
(Bid Round Data Package – BRDP)
Katika kifurushi hiki kuna
vitabu vya zabuni pamoja na maelekezo ya taratibu za kushiriki na kuwasilisha
zabuni [Bidding Instructions]; maelezo ya jinsi ya kutathini zabuni [Evaluation
Criteria]; vipengele vya tathmini ya uwezo kifedha [Fiscal Terms];
mfano wa mkataba wa kugawana mapato wa 2013 [Model Production Sharing
Agreement]; Sheria inayosimamia utafiti na uzalishaji ya mwaka 1980 [Petroleum
(Exploration and Production) Act 1980]; Sheria ya Hifadhi ya
Mazingira [Environmental Management Act 2004]; Sera ya Nishati ya 2003 [Energy
Policy of 2003]; na Sera ya Gesi Asilia ya 2013 [Natural Gas
Policy].
Sababu za kuuza data
Data za utafutaji mafuta na
gesi huuzwa kwa sababu gharama za kukusanya data ni kubwa sana, hivyo mauzo
hufidia gharama za ukusanyaji data hizo za awali na kufanya miradi ya
ukusanyaji data kuwa endelevu.
Kwa upande wa baharini
inabidi kukodi meli maalumu zenye mitambo ya kukusanyia data. Meli hizi
zinabeba mitambo na kompyuta maalumu zinazotumia teknolojia ya hali ya juu
kurekodi tabia za miamba za kuakisi mawimbi ya sauti chini ya ardhi (reflection
seismic methods). Meli hizi huweza kukaa baharini kwa
hadi miezi mitatu au zaidi zikifanya shughuli za ukusanyaji data na
zinahudumiwa kimahitaji kwa kutumia helikopta na meli ndogo za kutoa huduma.
Ulinzi pia kujikinga na maharamia huhitajika. TPDC na wabia wake hugharamia
zoezi la ukusanyaji data. Ni wazi kwamba gharama hizi huwa ni kubwa sana, hivyo
inabidi data zinazopatikana ziuzwe ili mwekezaji na TPDC waweze kurejesha
gharama zao.
Kwa upande wa nchi kavu
napo pia gharama ni kubwa. Gharama huanza kwa kutengeneza mikuza, kulipa fidia,
kulipa makandarasi wa kipima mikuza, kusafisha mikuza na kurekodi tabia za
miamba za kuakisi mawimbi data za mitetemo.
Tunahitaji makampuni
yatumie data hizi kutathmini sehemu ambazo zinaweza kuwa na hifadhi za mafuta
na gesi asilia. Tathmini hizo zitatumika kusaidia wataalamu kupima uwezo wa
makampuni na kuchagua kampuni stahili kupewa vitalu.
Utazamaji wa
Takwimu/ Taarifa - Data Viewing
Utazamaji wa taarifa za
kijiofizikia na kijiolojia (data viewing) unaweza kufanywa kwenye ofisi
za Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC). Mtazamaji anapaswa kuweka
miadi „appointment‟ ya
kutembelea chumba chenye hizo taarifa kupitia:
Shirika la Mendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC)
Tower
A, Benjamin William Mkapa, Pension Towers Building, Plot 23/90-23/92
Azikiwe/Jamhuri Streets,
Dar Es Salaam,
Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania
Simu ya mezani : +25522 2200103/4
Barua
pepe : tpdc4thround@tpdc-tz.com
Tovuti : www.tpdc-tz.com/tpdc/
Mtazamaji atapata nafasi ya
kuona taarifa zilizomo kwenye kifurushi cha zabuni cha vitalu vya bahari kuu (BRDP),
kifurushi cha zabuni cha Ziwa Tanganyika, „data‟ za
lazima za mitetemo zenye jumla ya kilometa 4500 za urefu, na taarifa nyinginezo
za mitetemo kama zitahitajika na pamoja na seti ya „data‟ za zamani zilizoboreshwa.
SEHEMU A: USHIRIKI
WA WAZAWA
Maelezo kuhusu fursa sawa
katika kushiriki kwenye mnada wa vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi ni kwa
mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004 (Public Procurement Act,
2002).
Ingawa zabuni iko wazi kwa
makampuni ya ndani na ya nje kushiriki, Utaratibu umewekwa utakaotoa upendeleo
kwa makampuni ya ndani yaliyosajiliwa kwa sheria za Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kumilikiwa na wazawa kwa
asilimia zisizopungua 50 ikiwa yatatimiza vigezo vilivyowekwa kuviwezesha
kupata huo upendeleo. Vilevile ushirikiano kiubia kwa makampuni yanayomilikiwa
na wazawa na yale ya nje utapewa upendeleo ikiwa utatimiza vigezo vilivyowekwa
ambavyo vinataka pamoja na mambo mengine; kuthibitisha kuwa atafanya kazi zenye
thamani isiyopungua asilimia 10 ya gharama ya kazi na kuwa atapata mgawo
usiopungua asilimia 20 ya faida itakayopatikana.
Mambo ya kufanya ili
kushiriki kwenye Zabuni
Kampuni inayotaka kununua
data na kushiriki kwenye zabuni inaweza kuwasiliana na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania,
Tower A, Benjamin William
Mkapa Pension Towers Building, Plot 23/90-23/92 Azikiwe/Jamhuri Streets,
S.L.P. 2774,
Tel:
+25522 2200103/4 Dar Es Salaam, TANZANIA
Barua
pepe: tpdc4thround@tpdc-tz.com
Wazabuni watarajiwa wanaweza kutuma maswali ya ufafanuzi
kuhusiana na zoezi la zabuni.
Muombaji anapaswa kurejesha kwa mkono nakala 2 pamoja na
nakala halisi vikiwa vimefungwa na kuviweka katika sanduku la zabuni lililopo katika ofisi kuu za Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (Tower “A”) chumba numbari 401 kilichopo
gorofa ya nne, jengo la Benjamin William Mkapa Pension Towers, Kitalu nambari
23/90-23/92, Azikiwe/Jamhuri Streets, Dar es Salaam, au itumwe kwa huduma ya
kutuma vifurushi vilivyoandikishwa (registered post/mail) kwenda kwa:
Katibu
wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania S.L.P. 2774,
Dar-es-Salaam.
Mshiriki katika zabuni pia
anaweza kushiriki katika zabuni kwa kuwasilisha zabuni yake siku ya ufunguzi
kabla ya saa nne asubuhi kwa masaa ya Tanzania siku ya Alhamisi tarehe 15 mwezi
Mei mwaka 2014 kama ilivyoelekezwa kwenye muongozo wa zabuni uliokwishatolewa
na unaweza kuuona kwenye tovuti maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya zabuni ya
ugawaji wa vitalu: http://www.tz-licensing-round.com
Tathimini za Zabuni
za vitalu zilizopokelewa
Zabuni za vitalu ni zabuni
za kimataifa na za wazi kwa makampuni yenye nia ya kufanya shughuli za
utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Zabuni hizo hazibagui asili ya makampuni,
kampuni yaweza kuwa ya kitaifa au ya kimataifa. Utoaji wa zabuni huzingatia
mambo makuu matatu:
·
uwezo
wa kampuni kifedha;
·
uwezo
wa kampuni kitaalamu; na
·
mgawo
wa rasilimali kwa Taifa endapo gesi na mafuta vitagunduliwa.
Zabuni zitakazopokelewa
zitafanyiwa tathmini kufuatana na vigezo vilivyowekwa kulingana na kazi za
kitaalamu ambazo muomba zabuni atakuwa ameahidi kuzitekeleza kwa vipindi vyenye
jumla ya miaka 11 (4/4/3) ya utafiti kama vilivyo kwenye sheria inayosimamia
shughuli za utafiti na uzalishaji wa mafuta na gesi Tanzania. Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika ataunda Kamati ya kufanya tathimini kwa mujibu wa sheria
inayosimamia manunuzi ya umma.
Mapendekezo ya Kamati ya
tathmini hupitiwa na Bodi ya Manunuzi ya Shirika ambapo mapendekezo ya Bodi ya
Manunuzi huwasilishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji ambaye naye huyawasilisha kwenye
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika ili kuandaa mapendekezo yatakayopelekwa kwa
Waziri kwani ndiye mwenye dhamana ya kutoa leseni za utafiti. Kama Waziri
atakubaliana na mapendekezo aliyoletewa ataiagiza kampuni iliyoshinda
itaarifiwe na kujiandaa kwa mazungumzo na timu ya washauri wa serikali kuanza
kwa nia ya kusaini mkataba wa kugawana mapato. Mkataba huu pindi unaposainiwa
pamoja na majukumu hutoa haki za kipekee kwa kampuni iliyoshinda zabuni kufanya
shughuli za kutafuta mafuta na gesi asilia kwa kipindi kilichowekwa katika eneo
husika.
Kampuni iliyoshinda hupewa
kuendesha leseni ya utafutaji na Waziri wa Nishati na Madini kwa niaba ya TPDC
kama mkandarasi. Kampuni hiyo itapaswa kufanya kiasi cha kazi za kitaalamu za
kitafiti zitakazohusisha shughuli za kijiofizikia,
kijiolojia na kijiochemia kama ilivyo kwenye mkataba.
Kazi hizo huhusisha
uchukuajia wa data za mitetemo za 2D na 3D, uchimbaji wa visima vya utafiti,
uchimbaji wa visima vya kuthibitisha kiasi ya hazina ya gesi au mafuta iliyopatikana
na pia uchimbaji wa visima vya uendelezaji wa maeneo hazina ilipogunduliwa.
Makadirio ya gharama za
mfano kwa kiwango cha chini kufanikisha shughuli za utafiti mpaka uendelezaji
zinaweza kuwa kama zilivyoainishwa hapa chini:
Dola
za
|
|
Marekani
|
|
Tathimini za kijiofizikia na kijiolojia
|
10
milioni
|
Ukusanyaji wa takwimu
za 2D na 3D
|
5 - 25 milioni
|
Jumla kwa Tathmini zote za kimazingira
(EIAs)
|
12
milioni
|
Uchimbaji wa visima 3 vya utafiti (@
170 mill)
|
510
milioni
|
Uchimbaji wa visima 6 vya tathmini (@
150 mill)
|
900
milioni
|
Uchimbaji wa visima 10 vya uendelezaji
(@ 100 mill)
|
1000
milioni
|
Jumla ya gharama isiyohusisha miundombinu
Dola za Marekani milioni 2437 (2.4 Bn)
Makadirio haya hayahusishi gharama za kuweka miundombinu
ya kuwezesha uzalishaji, usafishaji, uchakataji, uuzaji na gharama zinginezo.
Gharama hizi zinaonesha makadirio ya gharama za awali za shughuli za utafutaji
wa mafuta na gesi asilia. Gharama za uendelezaji kuweka miundombinu hadi
kufikisha gesi kwa mtumiaji huweza kufikia hadi Dola za Marekani bilioni 15
(US$ 15Bn).
Baada ya kusainiwa kwa mkataba, mshindi wa zabuni
atatakiwa kutekeleza mambo aliyoahidi wakati wa vipindi vya utafiti.
Akichimba kisima na
kugundua mafuta au gesi, atapaswa kufanya utafiti zaidi ili kujiridhisha kuwa
kiasi kilichogunduliwa kinaweza kuzalishwa kwa faida. Katika utafiti huo,
mwenye leseni analazimika kuchimba visima zaidi pamoja na kufanya thathmini za kijiofizikia
na kijiolojia zaidi.
Akijiridhisha, kuwa hazina
iliyogunduliwa inaweza kuzalishwa kwa faida, anapaswa kuomba leseni ya
uzalishaji ambao hutakiwa kuambatanisha maombi yake na mpango kabambe wa
kuendeleza hazina iliyopo (mafuta au gesi). Waziri akiridhika na mpango
uliowasilishwa na kampuni, huipa hiyo kampuni leseni ya uendelezaji inayompa
haki mwenye leseni kuendeleza na kuizalisha hazina aliyoipata kwa kipindi cha
miaka 25 na inaweza kuongezwa kwa kipindi kingine cha miaka 20.
Mauzo ya kinachozalishwa
hutumika kurudishia gharama zilizowekezwa kwenye shughuli zote za mradi na
faida hugawanywa kwa namna iliyokubalika katika mkataba wa kugawana mapato.
Taarifa hii inatolewa ili
kuelimisha umma kuhusiana na zabuni za ugawaji wa vitalu iliyozinduliwa tarehe
25/10/2013 na haipaswi kuchukuliwa kama maelekezo kwa wanaotaka kushiriki
kwenye zabuni (Invitation to Bid). Maelekezo ya namna ya kushiriki
kwenye zabuni yanapatikana kwenye mtandao ufuatao:
Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) linayaalika makampuni ya wazawa yenye uwezo wa kifedha
na kitaalamu kushiriki katika zabuni iliyotangazwa ya kutafuta wawekezaji wa
vitalu vya utafiti sambamba na makampuni ya nje.
Kwa maelezo zaidi
wasiliana na:
Idara ya Utafutaji, Uzalishaji na Huduma za
Kiufundi, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
Tower A, 9th Floor; BWM Pension Tower Azikiwe/Jamhuri
Street
P.O. Box 2774
Dar es Salaam, Tanzania simu:
+255 22 2200103/4, 2200112
fax: +255 22 2200113
Barua pepe: tpdc4thround@tpdc-tz.com
No comments:
Post a Comment