Kuro jike.
Kuro dume.
Ndugu zangu,
Nchi yetu imejaaliwa wanyama wengi wa mwituni ambao ni fahari kubwa kuwatazama kwa jinsi wanavyovutia.
Mnyama aina ya Kuro ama Waterbuck ni miongoni mwa hao wanaopatikana kwenye hifadhi zetu.
Nimewaona katika Hifadhi ya Serengeti, Tarangire na Arusha.
Kuro ni mnyama anayetokea katika Himaya ya Animalia, Faila ya Chordata, Kundi la Mammalia, Oda ya Artiodactyla, Familia ya Bodivae na Familia ndogo ya Reduncinae, Jenasi ya Kobus na Spishi ya K. ellipsiprymnus. Kwa jina la kisayansi anajulikana kama Kobus ellipsiprymnus.
Kuro (Kobus ellipsiprymnus) ni swala mkubwa ambaye anapatikana zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara, hivyo Tanzania tunayo bahati ya kuwa na wanyama hawa.
Ana urefu wa sentimeta kati ya 120 hadi 136 kuanzia begani wakati ukimpima kutoka kichwani ana urefu wa sentimeta kati ya 140 hadi 240.
Kuro madume wanakuwa na uzito wa kilogramu kati ya 200-300 ambapo rangi yao ni kijivu na inaweza kuwa nyeusi kadiri wanavyokua; wana mstari mweupe kwenye makoo yao na nyuma.
Tezi zao za kuzuia jasho zinasababisha watoe harufu fulani isiyoridhisha kwenye nyama yao, ukitaka kumla lazima umchune kwa tahadhari sana.
Madume pekee ndio wanakuwa na mapembe.
Majike huwa wanakuwa kwenye makundi ya kati ya wawili hadi 600 wakati madume wanatengeneza himaya ya ukubwa wa ekari 300 wakati wanapotaka kukutana. Hata hivyo, hupoteza himaya zao kabla hawajafikia umri wa miaka 10.
Nisiwamalize utamu, njooni wenyewe hifadhini mweze kujifunza.
Ndugu yenu Mhifadhi Mwandamizi,
Daniel Mbega
No comments:
Post a Comment