Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 13 December 2013

HAWA NDIO VIBAKA WA SERENGETI






Vibaka wapo, hata porini, ingawa inategemea ni vibaka wa aina gani.
Huku mijini tumezowea kuona vibaka wakikwapua na hata wengine wakichomwa moto. Lakini hali ni tofauti na hifadhini, hasa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mbali ya kupiga kelele kuhusu majambazi au majangili yanayopopoa maliasili za taifa hili - vita inayoendeshwa kwa nguvu zote za serikali - lakini wakazi wa pale Seronera yalipo makao makuu ya hifadhi hiyo, wanakabiliwa na changamoto ya 'vibaka'.
Vibaka hawa siyo binadamu, bali ni ngedere (Chlorocebus pygerythrus) na nyani, wakati mwingine ndege wakubwa aina ya korongo (Greater adjutant stork).
Ngedere ni wajanja sana, wanawaotea wakazi wa hapa wakitoka tu huku wakiwa wameacha milango ama madirisha wazi, basi wao wanazama ndani na 'kuiba' chakula - hasa ndizi, nyama na kadhalika.
Ndivyo pia wanavyofanya nyani. Lakini nyani wanakwenda mbali sana, kwani ikiwa watakuwa wamezowea eneo husika, basi wanajenga kiburi na kujifanya wababe kuliko binadamu.
Wanaoonewa zaidi ni wanawake, kwa sababu, kwa mujibu wa muhifadhi Miraji, wakati mwingine wanaweza kuwachapa makofi akinamama na watoto na kuwapora chakula.
Korongo nao wanapatikana mpaka kwenye makazi ya binadamu. Ingawa wao wanatafuta wadudu, bado hii haiwazuii kudokoa vyakula ikiwa tu wahusika wataacha wazi bila kufunika.
Mara kadhaa nilipata chakula kwenye kahoteli ka Impala hapo Seronera, ambapo nilishuhudia akina dada wakijitahidi kuwafukuza korongo kama wanavyowafukuza kuku. Maisha mengine ni raha sana jamani, onjeni muone.
Ngedere wanatokea katika Domeni ya Eukaryota, Himaya ya Animalia (Wanyama), Faila ya Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni); Ngeli ya Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha watoto wao), Oda ya Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu), Nusuoda ya Haplorrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na kima), Oda ya chini ya Simiiformes (Wanyama kama kima), Oda ndogo ya Catarrhini (Kima wa Dunia ya Kale), Familia ya juu ya Cercopithecoidea, Familia ya Cercopithecidae (Wanyama walio na mnasaba na kima), Nusufamilia ya Cercopithecinae (Wanyama wanaofanana na kima), Kabila ya Cercopithecini (Kima), na Jenasi ya Chlorocebus (Ngedere). Spishi zake ni C. aethiops (Linnaeus, 1758), C. cynosyros (Scopoli, 1786), C. djamdjamensis Neumann, 1902, C. pygerythrus F. Cuvier, 1821, C. sabaeus (Linnaeus, 1766), C. tantalus Ogilby, 1841.
Ngedere au tumbili ni wanyama wa jenasi Chlorocebus katika familia Cercopithecidae. Wanatokea Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, lakini spishi kadhaa zimewasilishwa katika sehemu nyingine za dunia.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment