Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 13 December 2013

NIMEPANDA META 2,720 ZA MLIMA KILIMANJARO


 Hapa ni Mandara Huts, meta 2,720 kutoka usawa wa bahari.

 Getini marangu kuingia Kilimanjaro National Park.
Niko tayari kupanda mlima.
Kibao kinatisha ati, lakini nakwenda.

 Baadhi ya wadau tukijiandaa kupandisha mlima. Wapo waliorudia njiani, lakini wapo waliotumia saa 6 kupanda. Mimi na Francis Godwin 'Mzee wa Matukio Daima' na Abdulkarim Mshana tulitumia saa 1:45 tu badala ya saa 3.
 Niko mbele zaidi, Francis Godwin anafuatia.
 Hawa ni wadau wengine tuliokutana nao wanarudi.
Mimi, Francis Godwin na Mshana.


Ndugu zangu,

Juzi Jumatano nimepanda Mlima Kilimanjaro. Sikufika kwenye kilele, lakini nimefika katika kituo cha Manadara Hut, ambacho kipo kwenye meta 2,720 kutoka usawa wa bahari. Ni historia kwangu na kwa familia yangu. Walau ndoto zangu zimekaribia kutimia, maana ninataka nifike Kilele cha Uhuru kwenye meta 5,895, niwe juu ya Afrika.
Mwendo wake kutoka geti la Marangu mpaka hapo ni kilometa 12 na ijapokuwa njia hii ndiyo inayosemwa kwamba rahisi kuliko zote za kupandia mlima huu, lakini hakuna kazi ngumu kama kupanda mlima.
Ndiyo, njia hii inajulikana kama 'Njia ya Coca-Cola' ambayo unaweza kuwa unapanda huku ukinywa Coca-Cola ama kutafuna chochote.
Muda uliowekwa pale wa kupanda hadi Mandara Hut ni saa 3, hata hivyo, mwenzenu nimefanikiwa kufika katika kituo hicho kwa kutumia saa 1.45 tu. Kushuka unapaswa kutumia saa 2, lakini nimetumia dakika 45 tu, tena basi nilikuwa nakimbia. Tulikuwa na wenzangu Francis Godwin, Abdul Mshana na Conrad Mpina.
Ndoto yangu ni kufika Uhuru Peak kwenye meta 5,895 kutoka usawa wa bahari ili niwe juu ya Afrika, lakini pamoja na wenzangu hatukuweza kuendelea kwa sababu wenyeji wetu walisema tuishie hapo Mandara.
Uwezo wa kusonga mbele nilikuwa nao, na kwa hakika nimeweza kuwatangulia wenzangu kwa umbali mrefu zaidi. Wapo niliowazidi kwa saa nzima, lakini wapo waliotumia saa 6 kupanda, na wakapelekewa gari mpaka nusu njia pale Kisambioni ili wateremke, maana nyonga ziligoma.
Hakika huu ni uzoefu mkubwa kwangu, hasa katika umri huu na shughuli tunazozifanya katika 'kusaka nyoka'.
Nimeziona changamoto nyingi, ambazo zinawajuza muda si mrefu.
Lakini ninawashauri thubutuni kupandisha Mlima Kilimanjaro, inawezekana kabisa.


Ndugu yenu,

Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment