Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 17 December 2013

UWANJA WA NDEGE WA SONGWE UITWE JOHN MWAKANGALE INTERNATIONAL AIPORT


Ndugu zangu,
Mimi nina mawazo. Katika kuweka kumbukumbu sawa za mashujaa wetu, walau wale wachache tu, ninapendekeza Uwanja wa Ndege wa Songwe Mbeya, ungeitwa John Mwakangale International Airport.

Sababu kubwa ya mapendekezo yangu ni kwamba, Mbeya ndiko wapigania uhuru wa Kusini mwa Afrika ambao baadaye walikuja kuwa viongozi wa nchi zao walipotua. Nelson Mandela kwa mara ya kwanza alitua Mbeya kabla ya kuja Dar es Salaam, aliyempokea ni John Mwakangale.
Mwakangale pia aliwapokea hapo Mbeya viongozi wengine akiwemo Sam Nujoma wa SWAPO (Southern West African Peoples Organization) wa Namibia, pamoja na wengine wengi.
Kwa maana nyingine, Mwakangale, pamoja na kumuenzi kwa kuuita Uwanja wa Maonyesho ya Nane Nane Mbeya kwa jina lake, ni kiongozi aliyesahaulika.
Hivyo basi, tusifanye makosa kwa kuubatiza uwanja huo jina la viongozi wetu wa sasa, hata kama uwanja huo umejengwa katika zama zao.
Ni ushauri tu, jamani.

Mzalendo mwenzenu,
Daniel Mbega
0655-220404

No comments:

Post a Comment