Baada
ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16
Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza
mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na
mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya
Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania.
Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.
Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.
Ningependa kuwaeleza Watanzania wenzangu yafuatayo.
Profesa Muhongo ni muongo
Imefika wakati wa Watanzania kubaini kwamba Mhe. Profesa Muhongo ni mtu mwenye hulka ya kusema uongo. Kwa mfano:
1. Kwenye kongamano la tarehe 8 Desemba 2013, Mhe. Profesa Muhongo
alisema kwamba moja ya kazi yake, alipokuwa akifanya kazi kama
mwanasayansi huko nje, ilikuwa kutabiri umuhimu wa sayansi katika uchumi
wa dunia miaka 3,000 ijayo. Huu ni uongo wa mchana kweupe.
2. Mnamo Julai 2012 Mhe.
Profesa Muhongo aliwaahidi Watanzania kwamba hakutakuwa na mgawo wa
umeme tena. Sote tunashuhudia mgao wa umeme ukiendelea hadi sasa.
3. Mnamo mwezi Septemba 2012,
Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akizungumzia mikataba ianayohusiana na
vitalu vya gesi akisema kwamba “baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na
inahitaji kuvunjwa” na “sitovumilia mikataba ambayo haina maslahi kwa
nchi na inawanufaisha wachache”. Baada ya hapo, Mhe. Profesa Muhongo
aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi
uliopangwa kufanyika mwezi huo na kupitia upya mikataba yote iliyokuwepo
awali. Sasa zaidi ya mwaka umepita na Mhe. Profesa Muhongo
hajarekebisha mkataba hata mmoja.
Profesa Muhongo na takwimu zake za maeneo ya madini
1. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu
Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Profesa Muhongo
alitoa takwimu za kuonyesha kwamba mimi ninamiliki eneo kubwa mara tatu
ya Dar es Salaam kupitia kampuni zangu tanzu.
2. Jumapili iliyopita mimi
nilimjibu Mhe. Profesa Muhongo kwa kumueleza kwamba takwimu zake kuhusu
mimi ni za uongo, na vilevile hizo alizotoa Bungeni pia ni za uongo na
nilimweleza kwamba swali la Mhe. Tundu Lissu lilikuwa ni “nani anamiliki
maeneo ya migodi”.
3. Katika eneo la kutafuta
madini unaweza ukapata au ukakosa – ni bahati nasibu, ndiyo maana maeneo
ya utafutaji yanakuwa makubwa. Vilevile wakati unatafuta madini
shughuli nyingine za wananchi waliopo katika eneo hilo huwa zinaendelea,
kwa mfano kilimo, makazi, uchimbaji mdogo mdogo nk. Unapopewa leseni ya
mgodi inamaana kwamba tayari umeshapata bingo – madini yapo na unaanza
kuchimba. Kwa mantiki hiyo maeneo ya migodi inakuwa midogo – isiyozidi
kilomita 10 za mraba, na shughuli zote za wananchi katika eneo hilo
zinasitishwa.
4. Sasa kwenye maelezo yangu ya
Jumapili iliyopita nilitamka wazi kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na
Watanzania wenzangu mgodi mmoja tu wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite
wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba. Profesa Muhongo
hajakanusha hili, badala yake anaturudisha Watanzania kule kule kwenye
maeneo ya utafutaji badala ya migodi.
5. Siyo hilo tu. Mhe. Profesa
Muhongo anafahamu kwamba kuna aina 6 za leseni za utafutaji na uchimbaji
wa madini. Lakini kwa makusudi kabisa Mhe. Profesa Muhongo anafananisha
leseni ya Mtanzania anayetafuta au kuchimba kokoto na leseni ya
mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba urani au dhahabu. Kweli
unaweza kufananisha kokoto na dhahabu?
6. Watanzania wanapaswa
kufahamu kuwa utafutaji madini (mineral prospecting) ndiyo msingi wa
maendeleo ya sekta ya madini kwa sababu bila utafutaji hakuna ugunduzi
na uendelezaji wa migodi hapa nchini. Lakini kuanzia Julai mwaka jana
Waziri Muhongo alipandisha tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na
500. Matokeo yake Watanzania wengi wanarudisha leseni zao na kasi ya
ugunduzi wa migodi imepungua.
7. Nia ya mtu inajionyesha siyo
tu kwa yale anayosema lakini bali pia kwa yale anayoacha kusema. Sasa
kama kweli nia ya Mhe. Profesa Muhongo ni nzuri, kwa nini hatoi takwimu
zinazohusu gesi? Kwa mfano, kwa nini hawaambii Watanzania kwamba:
a. Eneo ambalo limeshatolewa
kwa ajili ya mafuta na gesi lina ukubwa wa kilomita za mraba 243,000
ambalo ni sawa na karibu robo ya eneo la Tanzania nzima au mara 175 ya
eneo la mkoa wa Dar es Salaam au eneo la mikoa 9 ya Dar es Salaam,
Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga na Kagera.
b. Kwa nini Mhe. Profesa Muhongo hataki kuwaambia Watanzania
kwamba hakuna hata mzawa mmoja anayemiliki kitalu cha kutafuta au
kuchimba mafuta na gesi?
c. Kwa
nini Mhe Profesa Muhongo hataki kuweka wazi kwamba vitalu vyote 27 vya
gesi ambavyo vinaanzia katika mpaka wetu na Kenya hadi mpaka wetu na
Msumbiji, vimegawiwa kwa wageni? Je, kugawa vitalu vyote vya gesi kwa
wageni siyo hatari kwa mustakabali wa usalama wa taifa letu?
d. Lakini cha muhimu ni kwamba Watanzania wafahamu kwamba gesi
ambayo imeshagunduliwa Tanzania inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 500
bilioni wakati dhahabu yote iliyokwishagunduliwa hadi sasa na bado
haijachimbwa inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 60 bilioni kwa bei ya
sasa ya dhahabu.
Kwanini Profesa Muhongo hawaambii Watanzania takwimu hizi?
Profesa Muhongo na kauli zake kwamba Watanzania hawawezi kushiriki katika mchakato wa mafuta na gesi
No comments:
Post a Comment