Tujikumbushe tunapomaliza mwaka kwa tafakuri hii ya kamanda Yona Maro...
From: Yona Maro <oldmo...@gmail.com>
Sent: Monday, February 6, 2012 10:41 AM
Subject: [wanabidii] Mimba na Siri ya Precious
Sent: Monday, February 6, 2012 10:41 AM
Subject: [wanabidii] Mimba na Siri ya Precious
Pregnancy
- Mimba ilitungwa baada ya baba
kutoa hongo kwa kimada
- Ili kuthibitisha kama ni mimba
kweli kimada akatoa rushwa kwa daktari ili apimwe harakaharaka kwa kuwa
kulikuwa na msongamano wa wagonjwa
- Kila alipoenda kliniki wakati
wote wa Ujauzito alitoa 'chai' ili ahudumiwe vizuri na wauguzi na madaktari
Baada ya Kujifungua
- Baada ya kujifungua aliendelea
kutoa hongo awe wa kwanza kuhudumiwa, mwanae awe wa kwanza kuchomwa sindano za
Chanjo n.k.
- Mwanae akaitwa 'Precious'
Elimu kwa Precious
- Kuandikishwa chekechekea akatoa
hongo ili Precious apate nafasi katika shule nzuri kwa kuwa nafasi zilikuwa
chache, Precious anaangalia
- Kuandikishwa shule ya msingi mchezo
uleule, Precious anaangalia
- Tena sekondari akatoa 'Chai' kwa
mwalimu wa Hisabati ili Precious apate alama nzuri
- Chuo kikuu Precious hali ikawa
ngumu, akagawa uroda kwa mkufunzi ili apate alama nzuri
Kazi
- Precious akagawa uroda ili apate
kazi, akapata
- Precious akatishiwa mara kwa mara
kufukuzwa kazi kutokana na utendaji mbovu kinga ikawa ni kugawa uroda
- Akatumia nafasi yake kwa manufaa
yake binafsi
- Kwa tamaa ya vitu vya thamani
kuliko mshahara wake akaendelea kupokea rushwa
Ndoa
- Kwa kuwa wazazi wake (baba yake)
hakuwa mwaminifu katika ndoa yake (Precious ni mtoto wa kimada), naye Precious
hakuona sababu ya kuwa mwaminifu ktk ndoa
- Watoto wake wote walifuata
mlolongo kama wa kuzaliwa kwake
KIFO
- Hata alipougua ghafla , hongo
ikatumika apate huduma bora lakini Mungu alimpenda zaidi
- Walipoenda kuchonga jeneza,
wakakuta kuna order nyingi ikabidi watoe 'Cha Juu' ili kuchukua jeneza
lilokuwepo tayari
- Wakati wa mazishi Kwaya
iliyotakiwa kuimba wakati wa Maombolezo ilikuwa na safari , ikapewa 'cha juu'
ili kuahirisha safari
MWISHO
Kwaya ikaimba na Kumsifia Precious
alivyokuwa 'mtumishi mwema wa Mungu', tena wakamwomba Mungu ampokee kwa mikono
miwili , amuepushe na Moto wa milele.
Risala ikasomwa, na kusifia
utumishi wake uliotukuka, tena kaacha pengo lisilozibika.
Take Home Message
- Wazazi 'huwapakaza' watoto wao
matope ya dhambi toka pale mimba inapotungwa hata baada ya kuzaliwa
- Watoto wote huakisi tabia
walizojifunza toka kwetu, kama wazazi (Observational Learning)
- Kama hatuwezi kuwa wawazi hasa
pale kaburini hata kwa mtu aliyekufa na sifa mbaya akasifiwa basi tunahalalisha
matendo mabaya aliyoyafanya marehemu.
- Ili Kupambana na Rushwa twahitaji
kuanzia wakati wa Ujauzito, mtoto azaliwe bila rushwa, akue bila rushwa n.k
- KWA LEO NI HAYO TU!!!
No comments:
Post a Comment