Askari wa mwisho wa kikosi cha Luteni von Tettenborn ndio
hawakupata madhara makubwa ya mashambulizi ya Wahehe, washukuru kutokana na
makosa ya ishara, vinginevyo wote wangeangamia katika kipindi hicho cha dakika
15 tu. Von Tettenborn, Feldwebel Kay na askari kama 20 hivi Wasudani wakahamia
upande wa kushoto wa eneo la mapigano na kutengeneza nusu duara kwa ajili ya
mashambulizi huku wakiwa wameumia. Wakiwa hapo walipandisha bendera ya
Ujerumani juu ya mti na kupiga mbinja ili kuwaita manusura wengine.
Wakati huo Wahehe waliendelea kuwakimbiza manusura na kushambulia kila waliyemuona mbele yao. Mkanganyiko ukaongezeka baada ya kuwasha nyasi.
Wakati huo Wahehe waliendelea kuwakimbiza manusura na kushambulia kila waliyemuona mbele yao. Mkanganyiko ukaongezeka baada ya kuwasha nyasi.
Mnamo saa 2:30 asubuhi hiyo, Luteni von Heydebreck, Luteni
Usu Wutzer na Murgan Effendi wakiwa na askari wao 12 walipenya na kuungana na
kikosi cha von Tettenborn. Von Heydebreck alikuwa anavuja sana damu kutokana na
majeraha mawili makubwa ya mikuki. Kwa kuwatazama tu watu hao, von Tettenborn
akatambua kwamba vikosi vyao vyote vilikuwa vimesambaratishwa na kikosi cha
silaha kutekwa, ambapo Mkwawa aliteka bunduki 300. Askari wa jeshi la
Wajerumani waliouawa siku hiyo walikuwa zaidi ya 500.
Ilipofika saa 3:00 Luteni Usu Thiedemann, akiwa na majeraha
makubwa ya moto aliingizwa kwenye kikosi cha Luteni von Tettenborn akiwa
amebebwa na askari waliokuwa wanafanya doria. Nyasi zilizokuwa zinaungua sasa
zilimtisha von Tettenborn na manusura wengine.
Hadi kufikia saa 10:00 jioni Luteni von Tettenborn alikuwa
amewakusanya majeruhi wengi na kuokota baadhi ya mizigo yao. Wahehe waliokuwa
wamepagawa kwa hasira pamoja na moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuteketeza
msitu viliifanya kazi ya kuwatafuta majeruhi wengine kuwa ngumu, hivyo wengi
waliteketea kwa moto. Von Tettenborn akaamua kuanza kurudi nyuma kabla
hajazuiwa na Wahehe.
Wakati wa usiku wa manane kikosi kilichokuwa na Luteni von
Tettenborn kikapiga kambi ng’ambo ya pili ya mto tofauti na mahali walipolala
kabla ya kuanza mapambano. Kikosi chake sasa kilikuwa na yeye mwenyewe na
Luteni von Heydebreck, ma-NCO watatu wa Kijerumani (ingawa Luteni Usu
Thiedemann alikufa baadaye njiani), maofisa wawili wa Kiafrika, ma-NCO 62 wa
Kiafrika, wapagazi 74 na punda 7. Kutoka hapo wakaanza kutembea hasa nyakati za
usiku kurudi nyuma ambapo walifika Myombo Agosti 29.
Hakuna takwimu halisi za idadi ya Wahehe waliokufa kwenye
vita hiyo ingawa makadirio ni kati ya 260 hadi 700. Kwa ujumla, Wajerumani
walikuwa wameshinda vita dhidi ya wakoloni, ushindi ambao ni wa kihistoria kwa
mtawala yeyote wa Kiafrika wakati huo dhidi ya Wazungu. Haya yalikuwa matokeo
mabaya zaidi kwenye vita katika historia ya ukoloni wa Wajerumani.
Jeshi la Wahehe halikuwa na haja ya kuhitimisha ushindi wake
kwa kuwafuatilia Wajerumani waliosalia ili kuwaangamiza kabisa. Badala yake,
kuanzia wakati huo wakaendelea kuishambulia misafara yote ya Wazungu.
Tutaendelea...
No comments:
Post a Comment