Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe
TAARIFA KWA UMMA
KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA WILAYA YA BUMBULI ndugu ABDI SHEKIMWAGA
CHADEMA
Kanda ya Kaskazini, inawatangazia umma wote kuwa, Ndugu ABDI SHEKIMWAGA
amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Bumbuli kuanzia 21
Desemba 2013.
Ofisi ya kanda, ilipokea nakala
ya taarifa na miniti ya kikao kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka
kamati tendaji ya wilaya/jimbo pamoja na nakala ya barua ya tuhuma
alizoandikiwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA ili ajieleze na kujibu, ikiwemo na
barua ya tarehe 12 Desemba 2013 aliyoandikiwa katibu wa mkoa kujulishwa
mapendekezo na hatua za kunusuru chama dhidi ya hila mbaya zilizokuwa
zinafanywa na ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu SHEKIMWAGA
alitoa maneno ya kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa kwa
viongozi na kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo.
Uongozi
wa Kanda baada ya kupitia taarifa hizi na baada ya kufanya kikao cha
pamoja na viongozi wa wilaya tarehe 21 Desemba 2013 huko wilaya lushoto
mkoani Tanga, unamtangaza ndugu SHEKIMWAGA kuwa kwa kukinisuru chama
dhidi ya tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma
dhidi yake, kwa ajili ya hofu na kutokuwa na imani kulikoonyeshwa na
viongozi na wanachama wenzake AMESIMAMISHWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA
KUANZIA TAREHE 21 DESEMBA 2013. Hatua hii ni ya kuzingatia pendekezo la
kamati tendaji ya wilaya/jimbo kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (c),
“amekoma kuwa kiongozi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa
masharti ya katiba, kanuni na maadili ua chama”.
Aidha
uongozi wa kanda, unaliagiza baraza la uongozi la mkoa ambayo ndio
mamlaka ya nidhamu kwa wilaya/jmbo kwa mujibu wa katiba ya chama ibara
ya 6.3.6 (a) sehemu (iV) kuwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA APEWE FURSA NYINGINE
TENA akiwa katika hali ya kusimamishwa uongozi kwa kuandikiwa barua
tena ya tuhuma dhidi yake na apewe muda wa kikatiba kujibu ama sivyo
hatua kali zichukuliwe dhidi yake.
Tuhuma hizo ni;
Kuamua
kwa makusudi kuzuia na kukwamisha kazi za CHAMA, programu ya CHADEMA ni
msingi. Ndugu SHEKIMWAGA ametoa maneno ya uzushi na upotoshaji kwa
uwazi mbele ya viongozi wenzake na maafisa wa kanda kuwa hayuko tayari
kufanya kazi ambayo yeyé aliitafsiri kuwa ina lengo la kumjengea mtu
fulani mtandao ndani ya chama. Hii ni kinyume na kanuni ya maadili ya
kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (viii)
Ametoa
lugha na matamshi yenye kuonyesha udini na ukabila mbele ya viongozi
wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa kaimu katibu wa CHADEMA mkoa
wa Tanga ndugu Jonathan Leonard Baweje kuwa ni Mkristo na ametokea mkoa
wa Kigoma hivyo hawezi kuwa katibu wa mkoa wa Tanga kwa sababu sio
muislam. Hii ni dhambi mbaya sana na ni kinyume na kanuni ya maadili ya
kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (iv), “Kiongozi
yoyote asijihusishe na vikundi vyovyote vyenye misingi ya ukabila,
udini, au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama au
miongozi mwa jamii kisiasa au kijamii”.
Amejitambulisha wazi
mbele ya viongozi wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa yeyé yupo
kundi la Zito Kabwe na atahakikisha CHADEMA inakufa Bumbuli iwapo
maamuzi ya kamati kuu ya kumvua uongozi Zito Kabwe hayatabadilishwa.
Kitendo hiki cha kujitengenezea makundi na upotoshaji ni kinyume na
kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya
10.1. (iv), “Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi
halali ya vikao vya chama”.
Amezuia kwa makusudi kazi za chama
na amekuwa akifanya hujuma dhidi ya viongozi wengine ambao wamekuwa
wakifanya kazi za chama. Sambamba na hili ametuhumiwa kuwa anashirikiana
na wapinzani wetu CCM katika kuhujumu chama na kwa kumwaga sumu na
maneno ya uongo. Kitendo hiki kimekuwa sababu ya kuzuka kwa migogoro
isiyokwisha katika jimbo la bumbuli na imeendelea kuvunja moyo na kuleta
mifarakano inayorudisha nyuma kazi za chama. Jambo hili ni kinyume na
kununi ya maadili ya uongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1
(ix), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya
kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama
wake”.
Taarifa hii inaenda
sambamba na ndugu ABDI SHEKIMWAGA kukabidhi vifaa vyote vya chama,
ikiwemo kadi za chama mpya zipatazo 400 zenye thamani ya Tshs 600,000
ndani ya siku TATU kuanzia tarehe ya taarifa hii kwa KATIBU WA CHADEMA
MKOA WA TANGA.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini
inaendelea kuonya kuwa haitavulia kabisa kuona CHAMA CHETU ambacho ni
tumaini kwa Watanzania wengi kikivurugwa na watu wachache wenye hila
mbaya na chafu. Aidha nitoe rai kwa WanaCHADEMA wote wa kanda ya
kaskazini na Watanzania wapenda haki na kweli wasiwe na hofu yoyote na
matukio haya ya kukisafisha chama maana hatuna budi kusafisha na
kufukuza bundi wote waondoke.
Imetolewa leo tarehe 23 Desemba 2013
Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.
Makao Makuu ya Kanda – Arusha, Tanzania:
Simu: +255 754 912 914
No comments:
Post a Comment