Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 13 December 2013

PROPAGANDA NYINGINE BWANA, KAMA MLIMA KILIMANJARO UKO KENYA, MBONA WENYEWE WANAKUJA KUPANDIA KWETU?

 Msururu wa wanafunzi kutoka nchini Kenya ukipandisha Mlima Kilimanjaro juzi Jumatano.


Kati ya nchi zinazoongoza kwa propaganda, basi Kenya inaongoza.
Hawa jamaa walianza kwa kununua kahawa yetu, wakaifanyia packaging na kusema ya kwao. Haikutosha, wakanunua Tanzanite yetu, wakatengeneza na kuipack ili kuipeleka Ulaya na kusema vito hivyo vinapatikana Kenya, jambo ambalo ni urongo.
Wameeleza hivi karibuni kwamba Nyumbu wa Serengeti ni wa kwao na kwamba wanapatikana kwenye Hifadhi ya Maasai Mara, kwamba wanakuja mara moja tu Tanzania, jambo ambalo pia ni urongo kwa sababu Serengeti ndiyo inayotengeneza asilimia 90 ya ecosystem yote. Tena wanyama hao wanakwenda kupumzia kwa miezi isiyozidi miwili tu Maasai Mara wakitokea Serengeti ambako ndiko mimba zinatungwa na ndiko wanakozaliana.
Lakini propaganda ya muda mrefu ni kule kujinasibu kwamba eti Mlima Kilimanjaro uko Kenya. Wamewadanganya wengi na watu wakadanganyika. Kila watalii walipokwenda huko waliuona mlima, hata hivyo wakashindwa kupanda kutokea huko.
Unajua walikuwa wanasemaje? "Hapa waweza uona tu mlima, lakini ukitaka kupanda inabidi uende kwa Tanzo!"
Ndiyo, watalii wao walioletwa na kampuni za utalii za huko walikuwa wanakuja, na wanaendelea kuja Tanzania, tena pale kwenye geti la Marangu. Zamani walikuwa wakiwatanguliza wapagazi wao kubeba mizigo ya watalii na kupita njia za panya kwenye ushoroba unaotumiwa na tembo, lakini sasa inabidi na wapagazi wapitie Tanzania.
Jana majira ya saa 9 alasiri nimekutana na kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kenya wakipanda mlima kupitia Marangu.
Nikajiuliza, hawa si ndio wamekuwa wakitangaza kuwa Mlima Kilimanjaro uko kwao, sasa kwa nini wanakuja kupandia huku kwetu?
Uongo mwingine haufai. Kilimanjaro itaendelea kuwa Tanzania tu, si mahali pengine, wao watabaki na Mlima Kenya. Vinginevyo, kama wanaweza, waung'oe na kuusimika Mombasa basi.

Wasalaam,
Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment