Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 20 December 2013

NEC YATANGAZA UCHAGUZI KATIKA KATA 27


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema uchaguzi huo utafanyika katika halmashauri 23 baada ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa.

Alizitaja kata hizo na halmashauri zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).

Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti (Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba), Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na Namikago (Nachingwea).

Kata nyingine ni Partimbo na Loolera (Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na Nyasura (Bunda).

Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9.

Alipoulizwa kama Kata ya Kisesa iliyopo Mwanza itaingizwa katika uchaguzi huo baada ya aliyekuwa diwani wake, Clement Mabina kuuawa na wananchi, alisema haitaingizwa katika uchaguzi huo.

Alisema utafanyika baada ya Halmashauri ya Ilemela kupeleka maombi ya kuomba uchaguzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI).

CHANZO: mabadiliko.com

No comments:

Post a Comment