Jana hiyo, gari limekwama kwenye tope. Masharobaro mtawaona tu.
Huku inabidi uwe na gari ya four wheel, haikwami hata kidogo.
Lori hili la Chuo cha Wanyamapori cha Mweka ndilo lililotupeleka eneo la Mabokoni kutazama viboko ndani ya hifadhi hii ya Serengeti.
Wanafunzi wa mafunzo ya cheti ya wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka wakibadilisha mawazo na wanahabari baada ya kuwatazama viboko katika eneo hili la Mabokoni.
Hawa ni viboko.
Ndugu zangu,
Leo hii tumemaliza ziara yetu kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na tumekuja kulala Mto wa Mbu tukijiandaa kwa ziara ya kutembelea hifadhi ya Tarangire, ambako kuna nyoka aina ya Chatu wanaokwea miti.
Hata hivyo, jana tulipata changamoto kubwa baada ya kukwama mara kadhaa kufuatia mvua iliyonyesha na kusababisha barabara kujaa tope nyingi.
Lakini kama wanavyosema, msafiri kafiri, tulijitahidi kusukuma gari kwa msaada wa wanafunzi wa Chuo cha Wanyamapori cha Mweka waliokwenda pia kujifunza mambo mbalimbali hifadhini humo.
Ilikuwa tushindwe kwenda katika eneo la Mabokoni ambako wanapatikana viboko na mamba wengi, lakini ilibidi lori la Chuo cha Wanyamapori cha Mweka lije lituchukue na kuturudisha mahali tilipokuwa tumekwama.
Tutazidi kupashana zaidi yanayojiri kwenye ziara hiyo.
Daniel Mbega
No comments:
Post a Comment