Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 24 December 2013

ZAWADI HIZI ZOTE ZENU, CHRISMAS NJEMA WADAU


Ndugu zangu,
Kwanza natoa shukran nyingi kwa Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kutujaalia uhai - uzima na afya mpaka kuiona siku ya leo na kuikaribia sikukuu ya Krismas kwa mwaka 2013.
Pili natoa shukran za dhati kwenu wadau wangu ambao kuendelea kuperuzi kwenu mtandao huu kumezidi kunipa nguvu ya kuendelea kuuendesha mpaka sasa. Ninawashukuru sana kwa kuniunga mkono na ninawaomba msichoke.
Yapo mengi yaliyotokea tangu tuliposherehekea Krismas ya mwaka 2012. Wengi kati ya walioisherehekea sikukuu hiyo hatunao tena kwa mapenzi ya Mungu. Wengine wapo, lakini hali haiwaruhusu hata kunyanyua mkono. Hata hivyo, wapo wengine wageni waliozaliwa katikati ya kipindi hiki.
Haya yote yanadhihirisha ukuu wa Muumba na kwa maana hiyo hatuna budi kumsifu na kumtukuza Yeye.
Kwa mukhtadha huo, nachukua fursa hii kuwatakia wasomaji wangu wote Heri ya Krismas. Hakuna haja ya kuangalia unavaa nini au unakula nini. Kikubwa hapa ni kuangalia uzima, ambao tunapewa bure na Mwenyezi Mungu. Hayo yote ni matokeo tu. Msife mioyo, wekeni tumaini lenu kwa Mungu. Kila kitu kinawezekana na sote kwa pamoja tunaweza kabisa kuuvuka mwaka huu na kuingia 2014.
Zaidi tunapaswa kuishi katika kicho cha kumpendeza Muumba wetu ili hatimaye tuweze kuziona Krismas nyingine zaidi.
Mungu awabariki sana.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment