Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 29 December 2013

WAZAWA WATENGEWE SEHEMU YA HISA MTAJI MBEGU HUSIKA, SIYO VITALU KWENYE UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI


Imeandikwa na Dk A. Massawe
Uwezo wa kifedha pekee unatosheleza kuwezesha wazawa kushiriki kwenye biashara ya uendelezaji wa vitalu vya mafuta ya petroli na gesi asilia hapa nchini. Wa kitaaluma sio lazima kwani huo hununulika sokoni. Hata wengi waliowekeza kwenye makampuni makubwa ya kimataifa husika kwenye uendelezaji wa vitalu vya mafuta ya petroli na gesi asillia duniani ni uwezo wa kifedha pekee walio nao.


Bahati mbaya ni kwamba Tanzania bado haina hata kampuni moja ya wazawa yenye uwezo wa kifedha hitajiki kuiwezesha kuwekezea mtaji mbegu wote husika kwenye uendelezaji  wa kitalu chochote cha mafuta ya petroli au gesi asilia popote 
pale duniani, hasa baharini ambamo mtaji mbegu hitajiki huwa mkubwa zaidi.

Uwezo yaliyo nao makampuni ya kizalendo ni kushiriki kwa kuanzia kuchangia sehemu kidogo tuu ya mtaji mbegu husika kwenye uendelezaji wa kila kitalu cha mafuta ya petrol na/au gesi asilia hapa Tanzania, unaohusisha makampuni makubwa ya kigeni yenye uwezo wa kifedha na kiuzoefu.

Kushiriki huko kungeyawezesha ya kwetu kujijengea uwezo wa kifedha na kiuzoefu hitajiki kuyawezesha kukua ndani ya biashara ya uendelezaji wa vitalu vya mafuta na/au gesi asilia hapa nchini, hadi kwingineko duniani.

Kinachoyafaa makampuni ya wazawa na wazalendo binafsi ni kutengewa sehemu ya hisa mtaji mbegu husika kwenye uendelezaji wa kila kitalu utakaohusisha uwekezaji wa makampuni ya kigeni hapa nchini, mradi tuu uwezo wa wazalendo kuchangia hiyo sehemu ya hisa mtaji mbegu husika uwe umehakikiwa na Serikali.

Hii ingewezesha wazalendo kushiriki kwenye vitalu vyote hapa nchini na kuihakikishia nchi kupata faida hata kama kati ya vyote, ni kimoja tuu kitakachozaa mgodi wenye faida.

Badala ya kuyakaribisha ya wazawa kushiri kwenye zabuni ili kugombea kitalu kimoja au viwili na yale ya kimatafa yenye uwezo mkubwa, Serikali ingekuwa imefanya vizuri kama ingeshauriana na wazawa ili kubaini ni kiasi gani cha hisa mtaji mbegu husika kwenye kila kitalu kati ya hivyo saba ambacho wazalendo wako tayari kukichangia ili kwenye zabuni ya kimataifa kiwe kimekwisha tengwa pembeni kama mchango mbegu na hisa kwa ajili ya wazawa.

Hii ndiyo njia pekee itakayowezesha watanzania wengi  zaidi kushiriki na kuiwezesha nchi yao kujipatia mapato makubwa zaidi kutokana na uendelezaji wa vitalu vyake vya mafuta ya petroli na gesi asilia unaouhusisha makampuni ya kigeni yenye uwezo mkubwa zaidi kifedha na kiuzoefu.
CHANZO: wanabidii

No comments:

Post a Comment