Watu wanaoshukiwa kuwa
wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wameshambulia wanakijiji karibu na
mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwaua watu 45.
Walioponea kifo waliambia BBC kwamba
washambuliaji hao walijidai kuwa walikuwa wamekuja kuwahubiria
wanakijiji kabla ya kuanza kuwafyatulia risasi kiholea.Wakati huohuo,wakazi pamoja na maafisa wakuu wanasema kuwa watu 200 waliuawa katika mashambulizi tofauti mapema wiki hii.
Mji wa Maiduguri na vitongoji vyake, haujaathirika sana na mashambulizi tangu kutangazwa kwa sheria ya hali ya hatari mwaka mmoja uliopita.
Maeneo ya mashinani ndio sasa hulengwa kwa mashambulizi
Serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na shinikizo ndani ya nchi na kimataifa kuongeza juhudi za kukabiliana na kundi la Boko Haram tangu liwateke nyara wasichana zaidi ya miambili wa shule mwezi Aprili.
Kundi hilo limekuwa likiendesha harakati zake tangu mwaka 2009 katika juhudi za kudai uongozi wa kiisilamu.
Maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi mbali mbali ikiwemo maafisa wa usalama.
'Wanakijiji wahadaiwa'
Washambuliaji waliingia katika kijiji cha Barderi, karibu na chuo kikuu cha Maiduguri viungani mwa mji wa Maiduguri, wakiwaambia watu kuwa walikuwa wamekuja kuwahubiria, lakini baadaye wakaanza kuwashambulia kwa bunduki.
Wapiganaji hao wamewahi kutumia mbinu kama hizi za kijanja kuwahadaa wanakijiji na baadaye kuwashambulia.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment