TAARIFA KWA UMMA
UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO NA KILIMANJARO
Katika toleo Na. 1734 la gazeti la Jambo Leo la tarehe 10 Juni, 2014 katika ukurasa wa tatu iliandikwa taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari “Utafiti wa gesi kuinufaisha Morogoro, Kilimanjaro”. Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakaazi wa mikoa tajwa watanufaika na ugunduzi wa mafuta na gesi uliofanywa na Kampuni ya Swala katika maeneo hayo.
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa ya kwamba Kampuni ya Swala imegundua gesi na mafuta katika maeneo ya Morogoro na Kilimanjaro sio sahihi. Ugunduzi wa mafuta hufanyika tu baada ya kuchimba kisima cha utafiti na hatimaye mafuta au gesi iweze kutoka yenyewe kutoka ardhini. Hatua ya kuchimba kisima cha utafutaji hutokana na tafiti mbali mbali za awali za mitetemo ya ardhi na kubaini kama maeneo hayo yana uwezekano wa kuwa na mafuta au gesi ama la. Hata kama eneo linaonesha dalili nzuri za awali ni lazima sehemu hiyo ichimbwe na matokeo yake ni kuwa na ugunduzi au la. Vilevile ugunduzi huo lazima uonyeshe kutoa kiasi cha rasilimali ambacho kinaweza kuzalishwa kibiashara (economically viable).
Kazi zilizofanyika mpaka sasa na Kampuni ya Swala katika maeneo ya Morogoro – Kilosa na Pangani - Kilimanjaro ni utafiti wa awali wa kukusanya takwimu za mitetemo na kubaini kama maeneo hayo yana kina (thickness) cha kutosha cha miamba tabaka ambayo utafiti wa mafuta na gesi unaweza kufanyika. Hivyo utafiti wa kina unaendelea ili kubaini kama kuna miamba mashapo (prospects) ya kutosha kwa ajili ya kuchimba kisima cha utafiti. Uchimbaji wa kisima hicho unaweza kutoa mafuta au/na gesi au maji matupu. Hatua ya uchimbaji visima
(WANABIDII)
No comments:
Post a Comment