Shule hiyo ina walimu wawili tu wa masomo hayo kati ya walimu 52 waliyopo katika shule hiyo.
Hayo yamefahamika baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete baada ya kufanya ziara ya siku moja katika shule hiyo na kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa shule Bwana Christopher Mafuru.
Mwalimu Mkuu huyo alisema kwamba,pamoja na ukosefu wa walimu wa masomo ya Sayansi, shule hiyo ina mradi wa upandaji miti kwa kuzingatia suala zima la utunzaji mazingira katika maeneo ya shule na makazi.
Shule hiyo ya Lumala imeshaotesha miche elfu kumi,kati ya hiyo miche 1,000 ni miche ya miti ya kivuli na maua.Mradi huo ni endelevu na utaendelea kupanda na kuotesha miti kadiri ya mahitaji ya shule.
Alisema kwamba mradi unakabiliwa na tatizo la ukame kutokananaukosefu wa mvuahali ambayo imefanya mradi huo kusimamisha kuotesha miti au miche katika mradi huo. Pamoja na changamoto hizo,shule ina mpango wa kuotesha miti zaidi ya 40,000 kwa mwaka 2014/2015.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais.
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment