Maafisa wa Qatar wanaaminika
kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na tishio la kupokonywa
uenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa Qatar 2022 kufuatia tuhuma za
rushwa .
Kamati andalizi ya michezo hiyo sasa inaaminika
kupania kufanya kila iwezalo ikiwemo kufuata mkondo wa kisheria, ikiwa
kura ya kuchagua mwandalizi wa kombe la dunia 2022,itarudiwa.Shutuma za ufisadi katika mchakato wa kupiga kura ya uwenyeji zilisababisha kuitishwa kwa kura nyingine ikiwa hila itaonekana kuwa ilifanyika.
Mwanasheria huyo kutoka Marekani anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake itimiapo Juni 9.
Rais wa Uefa, Michel Platini, aliyeipigia kura
Qatari, alisema kuwa atakubali kufanyike kura ya marudio iwapo shutma za
ufisadi dhidi ya Qatari zitathibitishwa.
Msimamo wake uko sawa na ule wa makamu wa rais
wa Fifa, Jim Boyce aliyesema kuwa hatakuwa na shida yoyote ikiwa
‘makubaliano yatakuwa ni kura ya marudio kufanywa.’Maafisa wa Qatari wanadai kuwa mtaji wa takriban pauni bilioni 23, mahsusi kwa ajili ya kombe la dunia la 2022, itapotelea mbali iwapo Fifa italipokonya taifa hilo la ghuba haki ya kuandaa michezo hiyo.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment