Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, akikabidhi mchango wake wa Shs. 700,000 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Vicoba jimboni mwake. ...................................................................................
WANACHAMA wa vikundi vya Vicoba vya Igunga na Amkeni Group katika Kata ya Ihemi wilayani Iringa wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kwa kuviwezesha vikundi hivyo mtaji kwa ajili ya kuwawezesha wanachama hao kukopeshana zaidi.
Mratibu wa Vicoba Mkoa wa Iringa, Thisiana Kikoti, alitoa pongezi hizo leo wakati uzinduzi wa Vicoba katika Kijiji cha Ihemi.
Kikoti alisema uanzishwaji wa vikundi hivyo ni jitihada za aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Monica Mbega ambaye alihamasisha kuanzishwa kwa VICOBA mkoani Iringa.
Katika Jimbo la Kalenga, hamasa ya kuanzishwa kwa vikundi hivyo imefanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Dk.William Mgimwa na sasa jitihada zinazofanywa na mbunge wa sasa Godfrey Mgimwa ni wazi zitafanikisha kukuza uchumi kwa wananchi.
Alisema lengo ni kuona inaanzishwa benki ya VICOBA kwa ajili ya kuwawezesha wananchi zaidi kiuchumi.
Huku kwa upande wake, Mgimwa mbali ya kuchingia kiasi cha Shs. 700,000 pia alisema ndoto ya mbunge aliyefariki wa jimbo hilo, ambaye ni baba yake mzazi, ilikuwa ni kuanzisha Benki ya Maendeleo katika Jimbo la Kalenga na kuwa tayari alianza kuandika andiko na suala hilo ataliendeleza.
Wakati huo huo, mbunge huyo ameahidi kuchangia kiasi cha Shs. 700,000 kwa vikundi vya Ihekima, Tugele na Imani vyenye wanachama 80 kwa ajili ya kuviwezesha zaidi.
Vikundi hivyo vina akiba ya Shs. 8 milioni tangu vilipoanzishwa mapema mwaka huu.
credit: matukiodaima
|
No comments:
Post a Comment