Ndugu zangu,
Mapenzi yanahitaji kujitoa kwa kila kitu kwa mwenzi wako. Ni kutoa na kupokea, siyo kupokea tu. Waswahili wanasema, 'Kupeana ni kikoa'!
Ni vizuri kila mmoja kutambua wajibu wake kwa mwenziwe, na inapotokea yakawepo makosa, shurti nyote ama yule aliyekosea, amtake radhi mwenzake. Ndiyo mapenzi yanavyotaka - unakiri makosa, unaomba radhi na ni vyema mkasameheana ili safari iendelee. Kukiri makosa siyo kukiri udhaifu, kwa sababu hakuna aliye mkalimifu ati.
Lakini katika jamii yatu ya Kiafrika, ambayo kwa karne zote imetawaliwa na mfumo dume, ni nadra sana kumkuta mwanamume akijirudi na kuomba msamaha kama kijana huyo kwenye picha.
Wanaume ndio wanaoongoza kuwakosea wenzi wao, lakini daima hata pale nafsi zao zinapoona kwamba kweli wamekosea, huwa wagumu kukiri makosa, jambo ambalo ni la hatari katika maisha ya ndoa na mapenzi kwa ujumla. Daima wao ndio wanaotaka waombwe msamaha tu.
Jamii inahitaji kubadilika.
Ndugu yenu,
Brother Danny
No comments:
Post a Comment