INNOCENT A.
NDAYANSE (ZAGALLO)
0755 040 520 /
0653 593 546
Makella
anawaamuru wenzake wawaue wanafamilia wote katika nyumba ya Mzee Ndaishimiye
isipokuwa Judith tu ambaye amempenda na anataka kumuoa. Ni mwanzo mbaya na
kumbukumbu za kutisha kutokana na mauaji yaliyotokea. Je, wenzake watatii? Ungana
na msimulizi wako…
Na
ilikuwa kama alivyoamuru. Ni Judith pekee aliyebaki hai. Ndipo Makella
alipomwamuru Judith kusimama, amri ambayo Judith hakuwa na budi kuitii, na
ndipo pia akashikwa mkono na kuburutwa
akipelekwa nje. Huko pia alikokotwa kama mzoga, akitembea kwa tabu kutokana na
kuishiwa nguvu mwilini. Angezipata wapi nguvu ilhali muda mfupi uliopita
ameshuhudia wazazi na ndugu zake wakiuawa?
Kwa
jumla hakuwa timamu kiakili. Athari za kisaikolojia ziliutawala ubongo wake.
Tukio la muda mfupi uliopita lilikuwa ni kama ndoto isiyopendeza akilini mwake.
**********
WALIPOFIKA
mbali kidogo, Makella aliwaambia wenzake, “Tangulieni…ninataka kuongea kidogo
na Judi.”
Wenzake
walimtazama kidogo na kutii maneno yake. Wakatangulia mbele, yeye akabaki na
Judith nyuma wakitembea taratibu. Kisha Makella akamshika mkono Judith na
kumtomasa kidogo kiganjani. Kisha akasema, “Sikia Judi, mtoto mzuri, tambua
kuwa uhai wako una maana kubwa sana kwangu, uhai wako ni zaidi ya mimi
ninavyojali kuwa hai! Niko tayari kufa kuliko kushuhudia wewe ukiuawa. Naomba
uniamini. Wewe haukupaswa kuuawa ingawa katika operesheni ya leo tulipaswa
kumuua kila Mtutsi tutakayemtia machoni. Lakini kwa amri yangu wewe umebaki!”
Kufikia
hapo alitulia kidogo na kumtazama Judith kwa makini akitarajia pongezi, jambo
ambalo Judith hakulifanya. Zaidi, aliuinamisha uso wake kwa majonzi, machozi
yakambubujika.
Makella
alimgusa begani na kusema, “Pole sana Judi. Usilie. Tulia mpenzi. Umepona kwa
sababu naujali sana uhai wako. Naujali uhai wako kwa kuwa nakupenda kwa dhati.
Mapenzi yangu kwako ni mapenzi kutoka moyoni.”
Walikuwa
wamekwishavuka nyumba zaidi ya nne kutoka kwao Judith na kwa ratiba yao ilikuwa
sasa askari hao wasitishe zoezi lao. Hivyo walikuwa wakirudi kambini.
Wakati
huo Judith alianza kurejewa na utulivu kichwani. Akawa amepungukiwa na woga kwa
kiasi kikubwa, badala yake hasira ndizo zikamjaa moyoni kwa kiwango
kisichokadirika. Isitoshe chuki dhidi ya Makella ilikuwa ikimtawala kwa kiasi
kikubwa. Akahisi kitu kama kaa la moto likimkwama kooni!
Alijua
kuwa ilimpasa sasa kupiga moyo konde na kuwa makini, akitambua fika kuwa
chochote atakachokifanya kinyume na mapenzi ya Makella kinaweza kuyagharimu
maisha yake. Huyu Makella amekuwa akimfuata kwa muda mrefu. Na haya maneno yake
anayomwambia hayakuwa kipimo sahihi kuwa ana mapenzi ya dhati, hapana. Kwa hilo
Judith hakutaka kujidanganya.
Kama
amekwishadiriki kuua watu kama vile kuua panya au mende na hata amediriki pia
kuwaua wazazi wake na wadogo zake, mbele yake, ni kipi kitamfanya asite
kummaliza yeye kama atagundua kuwa bado hapendwi? Makella ni mtu mwenye moyo wa
binadamu au mnyama?
Akilini
mwake alimchukulia Makella kama binadamu mwenye akili ya mnyama japo alikuwa na
viungo vya kawaida, akizungumza kama binadamu wa kawaida na akivaa kama
binadamu wa kawaida Hivyo, jambo moja aliamua kuliwekea nadhiri; kuwa tayari
kuilinda heshima yake hata kama itabidi kuyagharimu maisha yake.
“Unasikia
mpenzi?” Makella aliendelea. “Wewe haustahili kufa! Wewe ni malkia wangu na ni
malaika wangu! Judi! Utakuwa mke wangu! Tutaishi maisha mazuri katika nyumba
yenye hadhi, nyumba nitakayokabidhiwa na serikali baada ya kufanya kazi hii kwa
ufanisi. Haya nd’o matunda ya kuwa mwanajeshi!
“Utakuwa
mke wa askari mwenye cheo cha juu. Hutasumbuka kwa kufanya kazi za ndani
zitakazouchosha mwili wako…hapana…kutakuwa na watumishi wanne watakaokuwa
wakifanya kazi za ndani na nje. Kazi yako kubwa ni kukaa na kucheki muvi, ukinywa bia au soda kwa raha zako,
basi! Jioni tunatoka na kwenda kupata nyama choma mahali huku tukishushia bia,
eti?”
Itaendelea kesho...
No comments:
Post a Comment