Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 8 June 2014

KWAYA YA UINJILISTI KKKT KIHESA IRINGA YAZURU SHAMBA LA WAZIRI MKUU PINDA ZUZU DODOMA

Kwaya maarufu ya Uinjilisti ya KKKT Kihesa mjini Iringa, iko mjini Dodoma kuchapa Injili ili mataifa waokoke. Kabla ya huduma hiyo muhimu ya kiroho, jana ilipata fursa ya kuzuru katika shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda lililoko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma, kujionea wenyewe shughuli mbalimbali za kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji wa mbuzi na nyuki. Humo kunalimwa nyanya, vitunguu, mboga mboga, migomba, mapapai na matunda mengine mengi, bila kusahau zao ambalo ni alama ya Dodoma, Zabibu. Hapa wako katika picha wakiwa wamepumzika baada ya kuzunguka kwenye shamba hilo kubwa. Wanasema 'ukienda hutamani kutoka' kutokana na mazao yaliyomo humo. Pengine walinyimwa' mahindi ya 'gobo' ambayo yamo humo, vinginevyo 'kila mtu angekuwa anatafuna' hapa.
Mwimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti ya KKKT Usharika wa Kihesa ya mjini Iringa akifurahia mandhari nzuri kwenye shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda huko Zuzu, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma. Wanakwaya hao wako huko kwa ajili ya kuhubiri Injili na kesho wanatarajiwa kutembelea Bungeni. ( Picha zote na msomaji wa www.brotherdanny5.blogspot.com)
Eti nyanya zinapatikana Ilula peke yake,nani kakudanganya?! Mmoja wa waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti ya Kanisa la KKKT Usharika wa Kihesa mjini Iringa akifurahia kuona matunda ya mbegu bora za nyanya kwenye shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda lililoko Zuzu, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.
 Mbuzi zaidi ya 100 wanafugwa kwenye shamba hili la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambalo liko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma. Ukiwa hapa utajifunza mambo mengi ya kilimo na ufugaji, kwani kilimo cha mazao mengi kimesheheni humo na kinaendeshwa na wataalamu kwa umwagiliaji.
 Siyo lazima usubiri ushauri wa daktari kwamba ule mapapai ndipo uanze kutafuta wapi yanapatikana. Katika shamba la Waziri Mkuu Mizengo Pinda lililoko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma, ameyapanda mengi na yanamwagiliwa kama hivi.
 Mahindi yamekauka kitambo Dodoma na watu wanavuna, lakini ndani ya shamba la Waziri Mkuu huko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma, hali ni tofauti kabisa. Bado 'gobo' inapatikana. Ni kutokana na kilimo cha umwagiliaji.
 Hata vitunguu vinastawi, tena kwa umwagiliaji. Ni ndani ya shamba la Waziri Mkuu huko Zuzu.
 Unadhani migomba inastawi Moshi, Mbeya na Kagera tu? Njoo Zuzu kwenye shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda uone. Mzuzu, Mshale, Bukoba na kadhalika zote zinapatikana hapa.
 Shamba hili lilikuwa na kokoto nyingi sana, kwa mujibu wa maofisa wanaolisimamia. Ingekuwa kama kule Iringa, 'wapwa' zangu Wanyalu wangeseme; "Bhe, unanipa shamba lenye kokoto litalifanyaje!" Lakini kokoto hizi zmechimbuliwa, shamba likasawazishwa tayari kwa kilimo. Matokeo yake ni kwamba, kokoto nazo ni dili la nguvu, kama hujengei wewe, unaweza kuziuza ukapata 'mpunga' wako, safi kabisa. Hili ni somo kubwa sana kwa Watanzania, hata wa hali ya kawaida, katika kupanga matumizi ya ardhi yao.
 Inahitaji mtaji wa kutosha kuhudumia shamba kama hili le Mhe. Waziri Mkuu Pinda. Nyenzo kama matrekta ni muhimu, lakini hata kama huna lako, waweza kukodisha.


 Halafu pia anafuga kweli nyuki. Ona mizinga ilivyopangana. Fursa zipo jamani, tuzikamate na kuzitumia na itawezekana ikiwa serikali nayo itawawezesha wakulima hata mitaji kupitia vikundi vyao.
Embe zimesheheni ndani ya shamba hili la Mhe. Pinda lilipo Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kumbe kila sehemu tunaweza kupanda mazao mbalimbali ikiwa tutazingatia ushauri wa wataalamu pamoja na kuwepo kwa miundombinu bora, hasa upatikanaji wa maji.
Jamani Dodoma aaaa, Dodoma ya Watanzania aaaa! Naam, na Zabibu ndilo zao kuu la biashara mkoani Dodoma ukiacha karanga na alizeti na Mhe. Mizengo Pinda naye alimelipa kipaumbele kwa kulima kitaalamu kabisa akitumia umwagiliaji wa matone kama kule Israel. Zao hili linastahimili sana ukame na kwa sasa lina soko kubwa mjini Dodoma ambako inaelezwa viko viwanda takriban vitatu vikubwa kabisa vinavyotengeneza mvinyo. Kwa kuwa malighafi ni zabibu, wananchi wanahimizwa kulima kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya viwanda hivyo. 










No comments:

Post a Comment