0712461976
KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakaa kesho Jumatatu (Juni 9 mwaka huu) kusikiliza rufani moja inayopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC.
Michael Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika juni 29 mwaka huu.
Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Julius Lugaziya itakutana saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam.
Wanachama wengi wa Simba na wadau wa soka kwa ujumla wanasubiri kuona nini kitatokea kesho katika kikao hicho. Swali kubwa ni je, Wambura atarudishwa kwenye uchaguzi au rafana yake itapigwa chini?
Majibu ni hapo kesho. Sinema kubwa ilitokea muda mfupi baada ya Wambura kuondolewa katika mchakato wa uchaguzi wa Simba. Wambura aliingia katika vita ya maneno na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Wakili Dkt. Damas Ndumbaro.
Wanaume hawa walishambuliana vikali na kuvuka mipaka na kuingia katika maisha binafsi. Wakacha mambo ya uchaguzi na kuanza kudhalilishana kwenye vyombo vya habari mpaka pale Wambura alipoamua kutumia busara yake.
Kwenye mkutano wa mwisho na waandishi wa habari, watu wengi walitegemea Wambura angejibu mapigo ya maneno mazito ya Ndumbaro, lakini aliendeshwa na busara na hapo sinema ikatulia.
Kusoma zaidi bofya www.blogspot.com
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment