Muigizaji mkongwe nchini,
Said ngamba al-maarufu ‘Mzee Small’ amefariki dunia usiku wa leo katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Taarifa
zilizotufikia zinaeleza kwamba Mzee Small alifikwa na mauti hayo majira ya saa
nne usiku wakati akiwa hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu.
Mipango inafanyika
nyumbani kwao Tabata.
Ni pigo lingine
tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii kadhaa majuma
yaliyopita.
Haifai kuhesabu,
lakini katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja tasnia hiyo imepoteza wasanii
takriban watatu. Ni hivi majuzi tu alifariki muongozaji filamu wa siku nyingi
nchini George Otieno 'Tyson' lakini kabla yake Adam Kuambiana alikuwa
ametangulia kwa kifo cha ghafla.
Mzee Small
amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miaka miwili.
Mzee Small alizaliwa
mwaka na alikuwa msanii maarufu wa maigizo
na vichekesho. Alikuwa mmoja wa wasanii
wakongwe nchini, hasa katika fani ya uchekeshaji ambayo sasa inachezwa zaidi na
vijana.
Mzee Small, ambaye aliwahi kushiriki katika
vikundi vingi vya sanaa kikiwemo DDC Kibisa, alizaliwa mwaka 1955 na kupata
elimu yake ya msingi katika shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Ndiye msanii
wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha katika luninga.
Mzee Small alikuwa anamiliki kundi la sanaa
linalojulikana kama Afro Dance ambalo
alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa
la Taifa, BASATA, na kupata usajili rasmi mwaka huohuo wa 1994,
ambapo pia aliwahi kwenda nalo Ujerumani katika tamasha kubwa la muziki la
WOMAD.
Mzee Small ameacha
mjane na watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike.
Mwenyezimungu
aiweke roho yake mahala pema peponi. -Amina.
No comments:
Post a Comment