Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 8 June 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA JUMAMOSI MANZESE MASHABIKI WASHANGILIA MWANZO MWISHO


Bondia Hassana Mlutu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Iddi Mustafa wakati wa mpamnano wao Mlutu alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Bondia Sako Mwaisege kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hussein Gobiso wakati wa mchezo wao uliomalizika kwa droo ya kufungana kwa pointi .


Bondia Hassani Mandula kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karim Migea wakati wa mpambano wao Mandula alishinda kwa k,o ya raundi ya pili .
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Mpambano wa masumbwi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ulioandaliwa na Kikosi cha Mizinga Entertainment ya jijini Dar es salaamumeleta chachu kwa mabondia mbalimbali baada ya wengi wao kuikubali kampuni hiyo na kuiunga mkono kwa kila hali, Mmoja wa wasisi wa kampuni hi ambaye niMsanii wa muziki wa hipop Karama Masoud ‘Kala Pina’  na Sempai Gola  wamehaidi kuwa bega kwa bega na mabondia mbalimbali kwa ajili ya kushiriki katika ngumi zitakazo pangwa tena hivi karibuniKatika mchezo huo bondia Salum Msabaha alimsambaratisha Shabani Hamisi, na George Epson akipewa kichapo na Mohamed Kambuluta na Mwinyi Mzee akitoa droo na Ismail Ndende ,Rashid Mohamed alimshinda Sadiki Nuru kwa pointi,Hassani Mandula akimsambaratisha bila huruma bondia Karim Migea kwa K,O ya raundi ya pili na Julias Kisalawe akitoa droo na Hassan Kiwale
Mpambano huo uliohudhuriwa na mashabiki lukuki  wakishangilia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wakati wa mapambano hayo,  kila mmoja alifurahia kuona  masumbwi hayo kutokana na kuwa na washiriki vijana  chipkizi wengi na wenye kuelewa nchezo wa ngumi.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment