Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 4 June 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AUNGURUMA MERERANI


1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini Mererani wilayani Simanjiro, Akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa upande mwingine kwa kushirikisha na wananchi, Huku akihimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimzia uhai wa chama, Katika ziara hiyo Katibu mkuu Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Akizungumza katika mkutano wa hadhara Kinana amesema atakuwa na kikao na viongozi wa chama cha  wachimbaji wadogowadogo kuhusu matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo katika shughuli zao. lakini pia akaongeza kwamba amewasiliana uongozi wa wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini ambapo wahusika wote watafika Mererani wiki hii ili kusikiliza matatizo wa wachimbaji hao na kuyapatia ufumbuzi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MERERANI)2Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini Mererani.2aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkurugenzi wa mgodi wa Suzan Didas Kenedy Limited   Bi. Suzan Kenedy  wakati alipotembelea mgodi huo ili ksikiliza kero mbalimbali zinazokabili wachimabji wadogowadogo wa madini huko Mererani Katikati ni Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro.3Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro akiwahutunia wananchi wa Mererani ambapo amewaeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na ambayo tayari imeshakamilika wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Mererani.5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akisoma makabrasha ya taarifa mbalimbali alizosomewa katika wilaya hiyo kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia wananch kutoka kushoto ni Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji na katikati ni  Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka.6Wananchi wakinyoosha mikono juu kuashiria kukubali jambo wakati mkutano huo.7Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji na Mbunge wa jimbo la Hanang akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiongozana na Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka wakati akiwasili katika mkutano wa hadhara viwanja vya CCM mjini Mererani.9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka alipokuwa  akitoa maelezo wakati Katibu mkuu huyo alipowatembelea wachimbaji wadogowadogo katika migodi ya Tanzanite huko Mererani.10Muonekano wa baadhi ya maeneo ya migodi ya Tanzanite inayomilikiwa na wachimabji wadogo huko Mererani.11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua migodi hiyo.12Kazi ikiendelea katika baadhi ya migodi.13Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa katika maeneo yao ya kazi.15Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akifuatana na Suzan Kenedy mkurugenzi wa kampuni Suzan Didas Kenedy Limited wakati akitembelea mgodi huo.16Wafanyakazi wa mgodi huo wakiwa kazini.17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipata maelezi kutoka kwa Suzan Kenedy Mkurugenzi wa Suzan Didas Kenedy Limited jinsi mtambo wa kuchimbia madini hayo unavyofanya kazi.18Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiendelea kutembelea mgodi huo kushoto anayemuaongoza ni Mkurugenzi wa kampuni Suzan Didas Kenedy Limited  Suzan Kenedy na kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka.19Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Naisinyai Mererani.20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua jengo la kituo cha afya cha Endiamtu Mererani.21Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa kituo cha afya cha Endiamtu Mererani.22Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa akina mama wa kata ya Kandasikira Mererani.23Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano katika kata ya Kandasikira.24Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kata ya Kadasikira Mererani.25Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu wakati alipozindua tawi katika kata ya kandasikira Mererani.26Baadhi ya wananchi wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika kata ya Lendanai na kuwasalimia hapo ndipo alipozaliwa Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro.27Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro akizungumza na wana Lendanai wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipowasili kijijini hapo, Mh.Ole Sendeka amezaliwa katika kijiji hicho.28Kikundi cha kwaya kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo.4Baadhi ya wananchi waliofurika katika mkutano wa hadhara mjini Mererani


CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment