WANAWAKE WAWILI WALIUAWA NA WAUME ZAO KATIKA MATUKIO MAWILI WILAYANI
CHUNYA. KATIKA TUKIO LA KWANZA LILILOTOKEA MNAMO TAREHE 06.02.2014
MAJIRA YA SAA 07:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA WILAYA YA
CHUNYA MKOA WA MBEYA MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGNES DAUD (32)
MKAZI WA KIJIJI CHA SHOGA ALIKUTWA AMEUAWA NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA THOMAS @MSUKUMA KWA KUMKATA KOROMEO KWA KUTUMIA KISU. MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA KIBANDA WALICHOKUWA WANAISHI NA MUME WAKE
KATIKA KAMBI YA UCHIMBAJI MADINI MALI YA ISACK MAMBO. KATIKA TUKIO LA
PILI LILILOTOKEA SIKU HIYO HIYO MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONIHUKO KATIKA
KITONGOJI CHA LONDON WILAYANI CHUNYA MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA DEFROZA GIDION (18) MKAZI WA KIJIJI CHA ISANZU ALIUAWA KWA
KUPIGWA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JANUARI. TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI
MAREHEMU AKIWA NYUMBANI. VYANZO VYA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI.
WATUHUMIWA WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
WALIPO WATUHUMIWA WA MATUKIO HAYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE
WENYEWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MWENDESHA BODABODA AFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO
LA KILIMO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.893
BPD AINA YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA EMANUEL NSOLO (31) MKAZI WA KIKONDO LILIMGONGA MWENDESHA
PIKIPIKI @ BODABODA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.322 CTJ AINA YA
SHINERAY AITWAYE OSWARD NDUNGURU (26) MKAZI WA IGANZO NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE AITWAYE GETRUDA CHARLES
MWAKALOBO (28) MKAZI WA IGANZO. MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA
AJALI NI DEREVA WA GARI KUKATISHA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE
MWENYEWE.DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
WATU WAWILI WAKAMATWA WAKIWA
NA NOTI BANDIA MKOANI MBEYA.
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA PATRICK MSIGWA (34)NA ANTHONY
MWAKIFWAMBA (32) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISYONJE WALIKAMATWA NA
WANANCHI WAKIWA NA NOTI BANDIA 57 @ TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 285,000/=.
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS
ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SIMAMBWE WILAYA YA MBEYA VIJIJNI BAADA YA
WATUHUMIWA HAO KUKAMATWA NA WANANCHI WAKATI WAKIWA WANANUNUA CHIPS NA
KUTOA NOTI MOJA YA TSHS 5,000/= NA WALIPOBANWA NDIPO WALIPOONYESHA NOTI
NYINGINE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO
KWA WANANCHI KUWA MAKINI WANAPO POKEA/TUMIA NOTI ILI KUEPUKA
KUTAPELIWA.NA NOTI BANDIA MKOANI MBEYA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment