Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika ulizuka majira ya saa 9:00 alasiri katika jengo hilo na kuzua mtafaruku mkubwa kwa askari na wanafunzi wanaochukua mafunzo ya Polisi.
Mkuu wa chuo hicho, Kamishana Msaidizi wa Polisi, Matanga Mbushi, ambaye alikuwa eneo la tukio pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema ni mapema mno kuzungumzia moto huo ila ni kweli umetokea.
“Nyote mmeshuhudia kweli moto umetekeza hili jengo na shughuli za kujaribu kuuzima ndiyo zinaendelea lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote hadi kesho tutakuwa tumewaandalia taarifa rasmi,” alisema mkuu huyo wa chuo kwa kifupi.
Gazeti hili lilifanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia wanafunzi wa chuo hicho na maofisa wa serikali wakijaribu kuokoa vitu mbalimbali kutoka katika jengo hilo ambalo baadhi ya vifaa hivyo viliteketea.
Vifaa vilivyoungua ni pamoja na sare za askari ambazo zimekuwa zikitumiwa wakati wa sherehe za kuhitimu mafunzo ya Polisi, viatu, kofia za Polisi, mikanda pamoja na magodoro yaliyokuwemo katika jengo hilo.
TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment